WAZIRI CHANA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU KAMISHNA MKUU WA HAKI ZA BINADAMU WA UMOJA WA MATAIFA
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na ujumbe wa Tanzania kwenye picha ya pamoja na Naibu
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Bi. Nada Yousseff Al Nashif, Julai 3, 2024
Geneva.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na
Lusajo Mwakabuku – WKS Geneva
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana akiambatana na ujumbe kutoka Tanzania
amefika katika ofisi za Naibu Kamishna Mkuu za Umoja wa Mataifa zilizopo Geneva
na kufanya mazungumzo na Bi. Nada Yousseff Al Nashif - Naibu Kamishna Mkuu wa
Haki za Binadamu juu ya utekelezwaji wa Haki za Binadamu nchini Tanzania.
Katika mazungumzo hayo, yaliyofanyika
Julai 3, 2024 Waziri Chana alielezea kwa kina juu ya suala malalamiko ambayo
Naibu Kamishna Mkuu alisema bado wanaendelea kuyapokea na kuyajadili kuhusu
kuhamishwa kwa nguvu kwa watu asilia (wamasai) katika maeneo ya Ngorongoro na
kusema kuwa kuwa Serikali iliamua kufanya maamuzi hayo kwa kuwa Wananchi wa
Ngorongoro walikuwa hawawezi kumiliki ardhi, kujenga makazi bora na ya kudumu
na kufanya mambo yao ya maendeleo kwa
ajili ya mustakabali wa familia zao kwa kuwa yalikuwa yanakinzana na Sheria ya
Uhifadhi.
Mbali na hilo, Dkt. Pindi
Chana amemweleza Kamishna huyo kuwa
wananchi wanaoishi Ngorongoro wamekuwa
wakikumbana na kadhia nyingi ambapo kuna wananchi ambao wameuawa na wanyamapori
wakali na waharibifu na wengine walijeruhiwa na wanyamapori hao na
kuwasababishia vilema vya kudumu.
Ameelezea kuwa wananchi
waliohamia kijiji cha Msomera wamelipwa fidia, wamejengewa nyumba zenye staha
pamoja na kupewa hati ya kumiliki ardhi pamoja na kupatiwa huduma zote za
kijamii ambazo walipokuwa Ngorongoro walizikosa
”Serikali imeendelea kuwapa
stahiki zao wananchi wote wanaohama kwa
hiari ikiwa ni pamoja na kuwapa fidia inayostahili pamoja na kuwasafirishia
mizigo, mali na mifugo yao kuelekea
kwenye makazi mapya na huu ndo msingi wa haki za binadamu” amesisitiza Mhe. Balozi
Dkt. Pindi chana.
Ameongeza kuwa “Wananchi wa Ngorongoro hususan watoto kwa kipindi kirefu walikosa haki ya kupata elimu bora, haki ya kuishi bila woga na haki ya kucheza kutokana na hofu ya kushambuliwa na wanyamapori wakali na waharibifu hivyo kitendo cha kuhamia Msomera watoto hao watapata haki zao za msingi kama ilivyo kwa watoto wa maeneo mengine.”
Comments
Post a Comment