WAZIRI DKT. PINDI CHANA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA SWITZERLAND
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana alipokutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Switzerland aliyemaliza muda wake nchini
Tanzania Bw. Didier Chasot. Julai 22, 2024 Dar es Salaam.
Balozi wa Switzerland aliyemaliza muda wake nchini Tanzania Bw. Didier
Chasot akifanya mazungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt.
Pindi Chana. Julai 22, 2024 Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana na Balozi wa
Switzerland aliyemaliza muda wake nchini Tanzania Bw. Didier Chasot kwenye
picha ya pamoja na baadhi ya maofisa kutoka ofisi hizo mbili baada ya kufanya
mazungumzo. Julai 22, 2024 Dar es Salaam.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana leo Julai 22, 2024 amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Switzerland nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Bw.
Didier Chasot.
Kikao hicho kilichofanyika
Jijini Dar es Salaam, kililenga kujadili namna ya kuendeleza mashirikiano katika kulinda haki za binadamu
hususan katika masuala ya uimarishaji wa utajiri asili na maliasilia za nchi,
kuendeleza na kulinda haki za binadamu na mapitio ya mfumo wa
haki za binadamu.
Comments
Post a Comment