WIZARA YAITA WADAU UBORESHAJI WA DAFTARI LA ORODHA YA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA
Msajili wa Watoa Huduma za
Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi akiwasilisha rasimu ya daftari la orodha
ya watoa huduma wa Msaada wa kisheria kwa wadau walioshiriki uboreshaji wa
Daftari la Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria. Julai 16, 2024 Dodoma.
Mdau Maiko Salali kutoka asasi ya Foundation for Disability Hope akichangia katika mjadala wa kuboresha Daftari la Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria leo tarehe 16/07/2024.
Leonard Haule ambaye anatokea
TAKUKURU lakini pia ni mwakilishi wa Chama cha Mawakili wa Serikali akichangia
katika mjadala wa kuboresha Daftari la Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa
Kisheria leo tarehe 16/07/2024.
Baadhi ya wadau wa kikao cha kuboresha Daftari la Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria wakifuatilia wasilisho la rasimu ya daftari la orodha ya watoa huduma wa Msaada wa kisheria leo tarehe 16/07/2024 Mtumba Jijini Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxx
Lusajo
Mwakabuku – WyKS Dodoma.
Wizara ya Katiba na Sheria leo
tarehe 16/07/2024 imeitisha kikao cha wadau kujadili uboreshaji wa Daftari la
Orodha ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria linalotarajiwa kuzinduliwa rasmi
mwishoni mwa mwezi wa nane, 2024.
Kikao hicho kilichofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba Dodoma,
kimejumuisha wataalam kutoka taasisi za Serikali na Asasi za Kiraia kimeazimia
kuunda timu maalum ambayo itatengeneza daftari lenye taarifa bora zaidi na
kuliwasilisha katika Menejiment ya Wizara kabla ya kuzinduliwa rasmi.
Lengo la daftari hili ni
kusogeza zaidi huduma kwa wananchi ili pale mwananchi atakapohitaji huduma za
Msaada wa Kisheria kutosafiri umbali
mrefu kufuata huduma hizo Wizarani na
badala yake kutumia daftari hilo kufahamu ni sehemu gani katika eneo alilopo
kuna huduma na aina ya msaada anayoweza kupata.
Comments
Post a Comment