Posts

Showing posts from August, 2024

Prof. KABUDI AWASILISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA SHULE YA SHERIA

Image
  Waziri wa  Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi (Mb) akiwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Sura ya 425 (THE LAW SCHOOL ACT CAP 425) katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Agosti 27, Bungeni jijini Dodoma. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akimpongeza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi (Mb) kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na pia kwa kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule  ya Sheria Sura ya 425 (THE LAW SCHOOL ACT CAP 425) katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Agosti 27, Bungeni jijini Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Johari akila Kiapo cha Uaminifu Bungeni na kukabidhiwa vitendea kazi na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Agosti 27, 2024 kabla ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa  Bunge la Jamhuri ya Muunga

KABUDI AFANYA KIKAO NA WAKURUGENZI NA MAOFISA

Image
  Waziri wa  Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi (Mb) Agosti 26, 2024 amekutana na kufanya kikao na baadhi ya Wakurugenzi na Maofisa  kutoka  Wizara ya Katiba na Sheria ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa   Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachotarajiwa kuanza Agosti 27, Bungeni jijini Dodoma.

SERIKALI INARIDHISHWA NA KAZI ZA WASULUHISHI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Abdallah Sagini akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi katika Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (Tiarb) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Protea Malliot jijini Dar es salaam, tarehe 23/08/2024. Rais wa Taasisi ya Usuluhishi Tanzania (TIArb), Madeline Kimei akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Abdallah Sagini aliyemwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi katika Mkutano wa Mwaka wa Saba wa  Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (Tiarb), 23/08/2024. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Abdallah Sagini akiwa meza kuu katika Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (Tiarb) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Protea Malliot jijini Dar es salaam tarehe 23/08/2024.              Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Abdallah Sagini akifuatilia matukio

KABUDI AANZA KAZI RASMI MOCLA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiongea na watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kupokelewa kuanza majukumu rasmi ya kuongoza Wizara hiyo, tarehe 20 Agosti, 2024 Mtumba Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akipokea nyaraka mbalimbali za utendaji kazi kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo ambaye sasa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ofisi za Wizara  Mtumba, jijini Dodoma, tarehe 20 Agosti, 2024. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) wakisaini nyaraka za makabidhiano ya ofisi katika Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria leo Agosti 20, 2024 Mtumba jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb.) akisaini kitabu  mara  baada ya kuwasili Ofisi za Wizara Mtumba, jijini Dodoma kwa ajili ya hafla ya makabidhiano ya Ofis

DKT. CHANA AWASILISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA SHULE YA SHERIA KAMATI YA BUNGE

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma, Agosti 14, 2024. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akichangia hoja wakati wa kujadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma, Agosti 14, 2024. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi akichangia hoja wakati wa kujadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma, Agosti 14, 2024. Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa wasilisho la Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria, katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma, Agosti 14, 2024. xxxxxxxxxxxxx

MASWI AFANYA MAZUNGUMZO NA MSHAURI ELEKEZI WA BSAAT

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi (wa tatu kulia) kwenye picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki kikoa na Mshauri Elekezi wa Programu ya BSAAT, Agosti 13, 2024 Ofisi za Wizara Mtumba Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi, 13 Agosti 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Mshauri Elekezi wa Programu ya Kujenga Uwezo wa Taasisi katika kupambana na rushwa (Building Sustainable Anti- Corruption Action in Tanzania - BSAAT). Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma, taarifa  ya utekelezaji wa programu hiyo iliwasilishwa na  kujadili maeneo ya mashirikiano kati yao na Wizara katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai.

DKT. CHANA AONGOZA KIKAO CHA WATAALAM KUJADILI SHERIA YA SHULE YA SHERIA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao cha Wataalam kupitia Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Sura ya 425 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, Agosti 13, 2024 Mtumba Jijini Dodoma.

PINDI CHANA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA USAJILI WA WATOTO DODOMA

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku - WyKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Agosti 09, 2024 amefanya ziara na kukagua zoezi la usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto wa umri chini ya miaka mitano katika hospitali ya St. Gemma, Kituo cha afya Makole na Zahanati ya   Kikuyu Jijini Dodoma. Katika ziara hiyo Waziri Chana, amewataka wananchi kuhakikisha watoto wao wanasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa mara baada ya kujifungua kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani. "Ndugu Wananchi hasa kina mama wenzangu, Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan imewaletea huduma hii ya vyeti vya kuzaliwa bure kwa watoto wetu hivyo hii ni fursa kwenu kwani vyeti hivyo vitawasaidia kupata huduma ya matibabu kupitia bima ya afya, baadaye elimu na ajira." Alisema. Pia Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana aliwakabidhi vyeti vya kuzaliwa baadhi ya akina mama waliojifungua salama na kuruhusiwa katika vituo hivyo vya tiba.

MSLAC YATWISHWA MGOGORO WA KIJIJI CHA BUMANGI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Butiama Mhe. Jumanne Sagini akihutubia wananchi wa Kijiji cha Bumangi, Agosti 07, 2024 Bumangi Butiama. Wananchi wa Kijiji cha Bumangi wakieleza kero zao kwa Mbunge wao Mhe. Jumanne Sagini kwenye mkutano wa hadhara, Agosti 07, 2024, Bumangi Butiama. xxxxxxxxxxxxxx William Mabusi – WyKS Butiama Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Butiama Mhe. Jumanne Sagini amewatwisha Wataalam wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia – MSLAC mgogoro wa kijiji cha Bumangi kilichoko Kata ya Muriaza Wilayani Butiama baada ya wanakijiji hao kunyang’anywa eneo lao la soko.   Uamuzi huo umefikiwa wakati wa mkutano wa hadhara kati ya Kijiji cha Bumangi na Mhe. Sagini Agosti 07, 2024. Katika mkutano huo wananchi walilalamika kunyang’anywa eneo ambalo hata ramani ya Kijiji inaonesha eneo hilo lilikuwa limetengwa kutumika kama soko.   “Hizi ni zama za utawala wa haki. Haikubaliki mtu kutumia uwezo na ushawishi wake kumnyima mtu mwingine haki,