Prof. KABUDI AWASILISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA SHULE YA SHERIA

 

Waziri wa  Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi (Mb) akiwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Sura ya 425 (THE LAW SCHOOL ACT CAP 425) katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Agosti 27, Bungeni jijini Dodoma.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akimpongeza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi (Mb) kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na pia kwa kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule  ya Sheria Sura ya 425 (THE LAW SCHOOL ACT CAP 425) katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Agosti 27, Bungeni jijini Dodoma.


Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Johari akila Kiapo cha Uaminifu Bungeni na kukabidhiwa vitendea kazi na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Agosti 27, 2024 kabla ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bungeni, jijini  Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba  na Sheria, Bw. Eliakim Maswi (kulia) akizungumza na Naibu Mwanasheria Mkuu wa  Serikali Bw. Samwel Maneno (kushoto) pamoja na baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo muda mfupi kabla ya kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Johari Agosti 27, 2024 Bungeni jijini Dodoma.

Katibu Mkuu  Wizara ya Katiba  na Sheria, Bw. Eliakim Maswi (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara na baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za Taasisi hizo wakifuatilia kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 27, Bungeni jijini Dodoma.



Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA