Posts

Showing posts from September, 2024

VIONGOZI WA DINI MNA DHIMA KUBWA KATIKA KUHAKIKISHA AMANI NA UPENDO NCHINI – KABUDI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na hadhara iliyojitokeza katika Mkutano Mkuu wa 53 wa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya   uliofanyika katika eneo la Kitongoji cha Kitonga, kata ya Msongola iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam tarehe 27/09/2024. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi na Shekhe Khawanja Muzaffar Ahmad Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahamadiyya Tanzania wakiswali dua ya jioni baada ya kushushwa kwa bendera ikiwa ni sehemu ya matukio katika mkutano huo. 27 Septemba, 2024 Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa ameambatana na Shekhe Khawanja Muzaffar Ahmad Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahamadiyya Tanzania na viongozi wengine wa dini ya kiislam wakiingia katika êneo la ukumbi ulipofanyikia Mkutano Mkuu wa 53 wa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya, 27 Septemba, 2024 Dar es Salaam. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo M...

PROF. KABUDI AFANYA KIKAO NA BALOZI WA URUSI NCHINI

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi leo 27 Septemba, 2024 jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya kikao na Balozi wa Urusi Nchini Bw. Andrey Avetisyan kujadili maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kidiplomasia kwa lengo la kuleta maendeleo kwa jamii. Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Kabudi amesema kuwa mbali na urafiki na ushirikiano uliopo baina ya Nchi hizi mbili wanaendelea kuangalia maeneo muhimu ya kuboresha ikiwemo ushirikiano kwenye masuala mbalimbali ikiwemo la utoaji wa huduma za haki ambalo liko chini ya mamlaka ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria, elimu, utamaduni, ulinzi, utalii, afya, biashara na uwekezaji. Aidha Bw. Avetisyan amesema kuwa Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuimarisha zaidi mahusiano yaliyopo ili kuboresha upatikanaji wa haki na kupambana na uhalifu kwa njia ya mtandao.

KITUO JUMUISHI TEMEKE KINABEBA DHAMIRA YA RAIS KATIKA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA HAKI NCHINI

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini alipotembelea Kituo Jumuishi  cha Masuala ya Familia Temeke jijini Dar es Salaam. Septemba 26, 2024. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akizungumza na baadhi ya Wananchi waliofika kupata huduma katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke jijini Dar es Salaam. Septemba 26, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini Septemba 26, 2024 alitembelea katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, ambapo katika ziara hiyo Naibu Waziri amejionea na kufurahishwa na huduma jumuishi  zitolewazo kituoni hapo. Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Sagini amesema kuwa Sekta ya Mahakama Nchini imeendelea kupiga hatua kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za utoji haki katika Vituo Jumuishi vya Mahakama Nchini. "Uwepo wa Kituo hiki hapa Temeke unaonesha dhamira ya dhati aliyonayo Rais wa...

SAGINI AIPONGEZA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA NA KUITAKA KUZIJENGEA UWEZO KAMATI ZA MAADILI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akizungumza na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (hawapo pichani) Septemba 23, 2024 jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (katikati) akiwa katika mazungumzo na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Septemba 23, 2024 jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu wa Tume Prof. Elisante  Ole Gabriel  na Naibu Katibu   wa Tume ya Utumishi  wa Mahakama Bi. Alesia Mbuya. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Septemba 23, 2024 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa na Naibu Katibu   wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Bi. Alesia Mbuya(kulia). xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Naibu Waziri wa Katiba na  Sheria Mhe. Jumanne Sagini (Mb), ameipongeza Tume ya Utumishi wa...

KATIBA NA SHERIA NA UONGOZI WA TLS WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiongea katika kikao na Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanzania (TLS) Mtumba Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria 17/09/2024. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi akiongoza majadiliano ya wataalam baina na Menejimenti ya Wizara na Uongozi wa TLS kabla ya kumkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria. 17/09/2024. Rais wa TLS Bw. Boniface Mwabukusi akielezea kufurahishwa kwake na mapokezi tangu walipowasili Wizara ya Katiba kabla ya kuanza kuelezea hoja za ushirikiano. 17/09/2024. Baadhi ya viongozi kutoka Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanzania (TLS) wakifuatilia majadiliano katika kikao hicho. 17/09/2024. Menejimenti ya Wizara na Uongozi wa TLS waliohudhuria katika kikao hicho wakifuatilia majadiliano. 17/09/2024. Waziri wa Katiba na Sheria, Menejimenti ya Wizara na Uongozi wa TLS wakiwa katika picha ya pamoja. 17/09/2024. xxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabu...

KABUDI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA AALCO THAILAND.

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba J. A. Kabudi aongoza ujumbe kutoka Tanzania nchini Thailand kushiriki Mkutano Mkuu wa 62 wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria wa Kimataifa wa Nchi za Asia na Afrika (AALCO). Septemba 11, 2024 Thailand. xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba J. A. Kabudi, Septemba 11, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Polcol Tawee Sodsong, Waziri wa Sheria wa Thailand ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia maeneo ya ushirikiano hususan kuwa na programu za mafunzo na kubadilishana uzoefu katika masuala ya sheria za uwekezaji na sekta ya sheria kwa ujumla. Waziri Kabudi anaongoza ujumbe kutoka Tanzania nchini Thailand unaoshiriki Mkutano Mkuu wa 62 wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria wa Kimataifa wa Nchi za Asia na Afrika (AALCO).

MOCLA YAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA MTEJA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja, Septemba 05, 2024 Mtumba Jijini Dodoma. Mkurugenzi wa Idara Katiba na Ufuatiliaji Haki Bi. Jane Lyimo akitoa neno la utangulizi kwa niaba ya Katibu Mkuu Bw. Eliakim Maswi katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja, Septemba 05, 2024 Mtumba Jijini Dodoma. Mkurugenzi Kitengo cha Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasili za Nchi DCP Neema Mwanga akitoa neno la ukaribisho kwa Wageni waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja, Septemba, 2024 Mtumba Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja, Septemba, 2024 Mtumba Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimsikiliza na kumhudumia mwananchi kutokea Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora aliyepiga simu katika Kituo cha Huduma kwa Mteja akiuliza kuhus...