KITUO JUMUISHI TEMEKE KINABEBA DHAMIRA YA RAIS KATIKA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA HAKI NCHINI
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini akizungumza na baadhi ya Wananchi waliofika kupata
huduma katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke jijini Dar es
Salaam. Septemba 26, 2024.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini Septemba 26, 2024 alitembelea katika Kituo Jumuishi
cha Masuala ya Familia Temeke, ambapo katika ziara hiyo Naibu Waziri amejionea
na kufurahishwa na huduma jumuishi zitolewazo kituoni hapo.
Akizungumza katika ziara hiyo,
Mhe. Sagini amesema kuwa Sekta ya Mahakama Nchini imeendelea kupiga
hatua kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika kuboresha
huduma za utoji haki katika Vituo Jumuishi vya Mahakama Nchini.
"Uwepo wa Kituo
hiki hapa Temeke unaonesha dhamira ya dhati aliyonayo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha jamii
inapatiwa ufumbuzi wa matatizo mbalimbali na haki inatendeka kwa kila mtu na
kwa wakati. Niwapongeze pia kwa kuwa katika kipindi cha miaka mitatu tangu
kuanzishwa kwa Kituo hiki mmeweza kufanya tathmini na kupata taarifa halisi
kuwa malengo ya kuanzishwa kwa Kituo hiki yamefikiwa kwa asilimia mia moja hii
ni hatua kubwa." Alisema Sagini.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa Kituo Jumuishi cha Temeke ni miongoni
mwa vituo sita Nchini Tanzania ambapo kwa ujumla wake vituo hivyo vinagharimu
kiasi cha Shilingi bilioni 51.45 vituo viwili vikiwa katika Mkoa wa Dar es
Salaam wilaya ya Temeke na Kinondoni, Vituo vingine vinne katika Mkoa wa
Morogoro, Dodoma, Mwanza na Arusha ambapo katika Kituo hicho Wananchi kati ya
800 hadi 1000 huudumiwa kwa siku.
Awali Naibu Waziri Sagini
alitembelea katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma na kuzungumza na Wananchi
waliokuwa wakipatiwa huduma ambapo Wananchi hao walikiri wazi kuwa Kituo hicho
kimekuwa na Msaada kwao kwa kuwapatia uelekeo wa masuala yanayohusu Ndoa,
Mirathi, Msaada wa Kisheria na pia kimewapa Wananchi nafuu kubwa kwani huduma
zote hutolewa bila malipo.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akizungumza na baadhi ya Wananchi waliofika kupata huduma katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke jijini Dar es Salaam. Septemba 26, 2024.
Comments
Post a Comment