PROF. KABUDI AFANYA KIKAO NA BALOZI WA URUSI NCHINI
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi leo 27 Septemba, 2024 jijini Dar es Salaam
amekutana na kufanya kikao na Balozi wa Urusi Nchini Bw. Andrey Avetisyan
kujadili maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kidiplomasia kwa lengo la kuleta
maendeleo kwa jamii.
Akizungumza katika kikao hicho
Mhe. Kabudi amesema kuwa mbali na urafiki na ushirikiano uliopo baina ya Nchi
hizi mbili wanaendelea kuangalia maeneo muhimu ya kuboresha ikiwemo ushirikiano
kwenye masuala mbalimbali ikiwemo la utoaji wa huduma za haki ambalo liko chini
ya mamlaka ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria, elimu, utamaduni, ulinzi,
utalii, afya, biashara na uwekezaji.
Aidha Bw. Avetisyan amesema
kuwa Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuimarisha zaidi mahusiano
yaliyopo ili kuboresha upatikanaji wa haki na kupambana na uhalifu
kwa njia ya mtandao.
Comments
Post a Comment