
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi akiongoza Kikao Kazi kilichowakutanisha Wizara, Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Kitengo cha Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu, tarehe 31 Oktoba, 2024 ofisi za Wizara Mtumba, Dodoma. xxxxxxxxx Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi katika kikao kazi kilichowakutanisha Wizara, Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Kitengo cha Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu kwa lengo la kujengeana uwezo wa utekelezaji wa masharti ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu, kikao kilichofanyika tarehe 31 Oktoba, 2024 katika ukumbi wa Wizara Mtumba, jijini Dodoma. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, kulijenga Taifa la Tanzania kunahitaji ushirikiano baina ya Taasisi mbalimbali na ni jambo lisilokwepeka hivyo ni vyema kukaa kwa pamoja ili kujua majukumu ya kila mmoja katika kutafuta mustakabali wa kuzuia biashara hiyo. Maswi amesema wap...