KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUFANYIKA MIKOA MINNE KWA PAMOJA
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester
Msambazi akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Makundi (Team Leaders) katika ukumbi
wa Hotel ya Edema Morogoro mjini tarehe 17/10/2024.
Wakili wa Serikali kutoka Katiba na Sheria Bw. Candid Nasua akifanya wasilisho katika mafunzo kwa Viongozi wa Makundi (Team Leaders) yatakayotoa msaada wa kisheria katika kampeni ya MSLAC katika ukumbi wa Hotel ya Edema Morogoro mjini tarehe 17/10/2024.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa Viongozi wa Makundi (Team Leaders) yatakayotoa
msaada wa kisheria katika kampeni ya MSLAC wakifuatilia wasilisho katika
ukumbi wa Hotel ya Edema Morogoro mjini tarehe 17/10/2024.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Wizara ya Katiba na Sheria ipo
katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuendeleza utekelezaji wa kampeni ya
msaada wa kisheria katika Mikoa Minne ambayo ni Mororgoro, Iringa, Songwe na
Mara.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi
wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi wakati
akimwakilisha Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria katika kufungua mafunzo ya siku
tatu kwa wataalam kutoka taasisi mbalimbali za kisheria ambao ndio watakuwa viongozi
wa timu zitakazotoa huduma ya Msaada wa Kisheria katika mikoa tajwa.
Comments
Post a Comment