KATIBA NA SHERIA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI UTEKELEZAJI WA MIKATABA YA HAKI ZA BINADAMU
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Haki za Binadamu Bw. Richard Kilanga akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kukamilisha taarifa ya Nchi ya kufuatilia utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa na Kikanda wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na Mkataba wa Haki za Wanawake Barani Afrika (Itifaki ya Maputo) tarehe 22 Oktoba, 2024 mjini Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Haki za Binadamu Bi. Beatrice Mpembo akizungumza
katika kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la
kukamilisha taarifa ya Nchi ya kufuatilia utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa
na Kikanda wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na Mkataba wa Haki za Wanawake Barani
Afrika (Itifaki ya Maputo) 22Oktoba, 2024 mjini Morogoro.
Baadhi ya Washiriki wakiwa katika kazi za vikundi wakipitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa na Kikanda wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na Mkataba wa Haki za Wanawake barani Afrika (Itifaki ya Maputo) tarehe 22 Oktoba, 2024, mjini Morogoro.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Wizara ya Katiba na Sheria
kupitia Idara ya Haki za Binadamu imewakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara
na Zanzibar katika kikao kazi cha kukamilisha taarifa ya Nchi ya kufuatilia
utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na Mkataba
wa Haki za Wanawake Barani Afrika (Itifaki ya Maputo).
Katika kikao hicho
kinachofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Oktoba, 2024 Flomi hoteli mjini
Morogoro, kitaandaa taarifa itakayoonesha ni kwa namna gani kwa mujibu wa
Mikataba tajwa Nchi ya Tanzania imefanikiwa kutekeleza viwango ambavyo Nchi
inapaswa kuvifuata katika kuendeleza na Kulinda Haki za Wanawake.
Itifaki ya Maputo imekuwa na
manufaa makubwa katika kuwezesha na kuendeleza upatikanaji wa Haki pamoja
na kuonesha jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutokomeza vitendo vya
unyanyasaji na ukatili dhidi ya Wanawake nchini Tanzania.
Tanzania ni miongoni mwa Nchi
ambazo zimeridhia utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na
Watu pamoja na Mkataba wa Haki za Wanawake barani Afrika (Itifaki ya
Maputo) yenye malengo ya kulinda Haki za Wanawake inayojumuisha Haki za
kushiriki katika siasa, kazi za kijamii ,Haki ya uzazi na kupinga mila potofu
kama vile ukeketaji.
Comments
Post a Comment