Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi akiongoza Kikao Kazi kilichowakutanisha Wizara, Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Kitengo cha Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu, tarehe 31 Oktoba, 2024 ofisi za Wizara Mtumba, Dodoma.
xxxxxxxxx
Wito huo umetolewa na Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi katika kikao kazi
kilichowakutanisha Wizara, Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanganyika
(TLS) na Kitengo cha Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu kwa lengo la
kujengeana uwezo wa utekelezaji wa masharti ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha
Haramu, kikao kilichofanyika tarehe 31 Oktoba, 2024 katika ukumbi wa Wizara
Mtumba, jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu,
kulijenga Taifa la Tanzania kunahitaji ushirikiano baina ya Taasisi mbalimbali
na ni jambo lisilokwepeka hivyo ni vyema kukaa kwa pamoja ili kujua
majukumu ya kila mmoja katika kutafuta mustakabali wa kuzuia biashara
hiyo. Maswi amesema wapo baadhi ya watu wasiowaadilifu ambao
wanaweza kushiriki kwa namna moja au nyingine katika utakatishaji fedha jambo
ambalo halikubaliki Kisheria.
Kamishna wa Kitengo cha
Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Bi. Fatma Simba amesema mapambano dhidi ya
biashara hiyo ni jambo linalohitaji nguvu ya pamoja kati ya pande zote na
madhara ya utakatishaji wa fedha haramu ni ya Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa na
Kiusalama ambapo huhatarisha Utawala wa Sheria na Usalama.
Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi amesema TLS ni chombo cha Kisheria na
Viongozi wake wameapa kuisimamia Katiba na Sheria na hawapo tayari
kusimama kama kizingiti cha kuzuia utekelezaji wa jambo ambalo linaleta maslahi
mema katika Taifa.
Comments
Post a Comment