WIZARA YATOA MOTISHA
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akikabidhi kiasi cha shilingi milioni sita kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Jaji Mstaafu Mathew
Mwaimu ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim
Maswi wakati alipotembelea makao makuu ya Tume ikiwa ni sehemu ya motisha kwa
ajili ya Watumishi wawili waliofanya kazi katika Tume kwa zaidi ya miaka
thelathini. 15 Oktoba, 2024 Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.
Comments
Post a Comment