TUME YA TEC YAKUTANA NA KABUDI NA KATAMBI
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John
Kabudi akifafanua jambo katika kikao
hicho pembeni yaka ni Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu walipokutana na Tume ya TEC Mtumba
Dodoma leo 07/11/2024.
Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu -
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akichangia hoja katika
mazungumzo hayo.
Jopo la wawakilishi wa Tume ya Kimisionari ya Baraza la
Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi na Mhe. Patrobas Katambi, Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamoja na
wajumbe wa menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Mwenyekiti wa Tume ya Kimisionari ya Baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Damian Dallu akifafanua jambo
katika kikao hicho.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Jopo la wawakilishi wa Tume ya
Kimisionari ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) limekutana na Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi na Mhe. Patrobas
Katambi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu kuzungumzia juu ya taarifa ya takwa la marekebisho ya sheria kuhusu
wamisionari wa kikatoliki Tanzania wenye uraia wa nje.
Mazungumzo hayo yanafuatia
ombi lililotolewa na Askofu Mkuu wa Songea na Mwenyekiti wa Tume ya Kimisionari
ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Damian Dallu kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara
ya kikazi na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini mjini Songea mwishoni mwa
mwezi Septemba mwaka huu Mkoani Ruvuma.
Mazungumzo hayo yamefanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba leo tarehe
07/11/2024 na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Bwana Eliakim Maswi na baadhi ya
wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.
Comments
Post a Comment