MSLAC KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KILOSA
xxxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Wilaya ya Kilosa imekuwa ikikabiliwa na migogoro mingi ikiwemo ya wakulima na wafugaji na kwamba imekuwa makao makuu ya migogoro ambayo mwarobaini wake ni Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia - Mama Samia legal Aid Campaign. Waziri Ndumbaro amebainisha hayo Desemba 15, mwaka huu wakati akizindua kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika kata ya Magomeni Wilayani Kilosa Mkoani humo ikiwa ni siku ya pili baada ya kampeni hiyo kuzinduliwa Kimkoa Disemba 13, 2024. Zaidi, Waziri huyo amesema migogoro inayowakabili wananchi wa Kilosa kumeifanya Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuteua Kilosa kuwa makao makuu ya migogoro ya wakulima na wafugaji, hivyo ameitaka timu ya wanasheria wa kampeni hiyo kuandaa ripoti itakayoonesha migogoro iliyotatuliwa na ambayo haijatatuliwa ili ambayo haijatatuliwa ifanyiwe oparesheni maalum ya siku kumi kuhakikisha inaisha. "Na mimi niseme sasa baada ya siku hizi k...