UZINDUZI WA SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU
Mgeni Rasmi Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi
nya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akisoma hotuba yake
katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu. Tarehe 5 Novemba, 2024
katika Ukumbi wa Ofisi za Takwimu Dodoma.
Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bw. Eliakim
C. Maswi, katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu na aliyepo kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Takukuru, Bibi Neema M. Mwakalyelye wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Maadili
na Haki za Binadamu. Tarehe 5 Novemba, 2024.
Naibu Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Dr. Franklin
Rwezimula (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Ikulu Mululi Majula Mahendeka
kabla ya kuanza maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu. Tarehe
5 Novemba, 2024.
xxxxxxxx
Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria ikiongozwa na
Katibu Mkuu Bwana Eliakim C. Maswi imeshiriki Uzinduzi Wa Siku ya Maadili na
Haki za Binadamu ulioadhimishwa. Tarehe 5 Novemba, 2024 katika ukumbi wa
mikutano wa Ofisi ya Takwimu Jijini Dodoma ambapo mgeni Rasmi alikuwa Mhe.
George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi nya Rais – Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora.
Comments
Post a Comment