WIZARA YAPOKEA MAGARI TISA KATI YA KUMI KURAHISISHA HUDUMA ZA KISHERIA KWA WANANCHI
Mwonekano wa magari tisa kati ya kumi yaliyopokelewa katika
Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa shughuli za
utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
20 Desemba, 2024.
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na
Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakishangalia na kumkabidhi tuzo
ya utendaji bora Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi mara baada ya Wizara
hiyo kushika nafasi ya pili katika Wizara zinazojali
maslahi ya Watumishi. 20 Desemba, 2024.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro amewataka watumishi wa wizara ya Katiba na Sheria
kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kutokana na Serikali kuweka mazingira
wezeshi kwa ajili ya kurahisisha utendaji wao wa kazi.
Waziri Ndumbaro ameyasema hayo
wakati akipokea magari tisa kwa ajili ya watumishi wa wizara hiyo katika
kutekeleza Kampeni maalum ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid
campaign.
Amesema magari hayo yatasaidia
kurahisisha utendaji kazi kwa Mikoa sita kwa wakati mmoja hivyo watendaji
kuendelea kuwa waadilifu.
Magari tisa kati ya kumi
yamezinduliwa tarehe 20 Desemba, 2024 ambapo lengo ni katika kurahisisha
shughuli za utendaji kwa watumishi wa wizara hiyo.
Comments
Post a Comment