JAPAN KUSHIRIKIANA NA WIZARA KUENDELEZA SEKTA YA SHERIA NCHINI
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.
Yasushi Misawa wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Wizara
Mtumba, jijini Dodoma tarehe 8 Januari, 2025 kwa lengo la kumuaga baada ya
kumaliza muda wake nchini.
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na ugeni kutoka Ubalozi wa Japan
nchini Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Yasushi Misawa wakati alipomtembelea
Waziri katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma tarehe 8 Januari, 2025 kwa
lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 8 Januari, 2025 amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa
alipomtembelea Mhe. Waziri katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma kwa
lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
Katika mazungumzo hayo
yaliyohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi, Naibu Katibu Mkuu
Dkt. Franklin Rwezimula na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara Viongozi
hao walijadiliana ni kwa namna gani mahusiano baina ya nchi hizo yamekuwa
yakiimarika katika sekta mbalimbali za kimaendeleo.
Kwa upande wake Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amempongeza Mhe. Balozi kwa
kazi kubwa aliyoifanya na amesema kuwa Tanzania inathamini ushirikiano uliopo
kati ya nchi hizi hususan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani
(JICA) ambalo limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri Ndumbaro ameongezea
kuwa yapo maeneo katika sekta ya Sheria ambayo Nchi ya Japan kwa kushirikiana
na Tanzania wanaweza kubadilishana uzoefu ili kuweza kusaidia Wananchi hususan
katika maeneo ya vijijini ikiwa ni pamoja na masuala ya upatikanaji haki pamoja
na utatuzi wa migogoro.
Kwa upande wake Balozi Misawa
amesema kuwa wataendelea kudumisha uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Japan
hususan katika sekta ya Sheria kwa kuwajengea uwezo Wataalamu na
kubadilishana uzoefu katika masuala ya utatuzi wa
migogoro na usuluhishi.
Comments
Post a Comment