WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA
Waziri wa Katiba na Sheria
Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 23 Januari, 2025 amewasili Mkoani Kigoma na
kukutana na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali
Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Thobias Andengenye, kwa ajili ya kushiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya
Msaada wa Kisheria ya Mama Samia utakaofanyika tarehe 24 Januari, 2025 Mkoani
Kigoma.
Akizungumza mara baada ya Mhe.
Waziri kuwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya salamu, Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma amesema kuwa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa
anayoifanya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila Mwananchi anapata Haki na kwa
wakati kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria.
Kwa upande wake Waziri wa
Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa kupitia Kampeni ya Msaada wa
Kisheria migogoro mbalimbali itakwenda kutatuliwa kupitia njia ya amani, usuluhishi,
Mahakama, kiutawala na kwa njia za kiuchunguzi.
Mhe. Ndumbaro amesema kuwa,
Kampeni ya Msaada wa Kisheria itatekelezwa kwa muda wa siku tisa katika
Halmashauri tisa za Mkoa wa Kigoma na kuwafikia Wananchi katika maeneo
mbalimbali ili kuhakikisha matatizo yote ya Kisheria yanapatiwa suluhu.
Comments
Post a Comment