WIZARA YAWAPIGA MSASA WARATIBU WA MSAADA WA KISHERIA NCHINI
Wizara ya Katiba na Sheria imetoa mafunzo kwa Waratibu wa
Mikoa na Halmashauri kuhusu utekelezaji
wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Mafunzo hayo yameanza
tarehe 14 Januari, 2025 katika Chuo cha Uongozi Mwl.
Nyerere Kibaha, Pwani.
Waratibu wa Mawakili wa Serikali, Wahadhiri Wasaidizi wa
Vyuo Vikuu na Mawakili wa Kujitegemea kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika
(TLS) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa
Waratibu wa Mikoa na Halmashauri kuhusu utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa
Kisheria ya Mama Samia. Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku mbili katika
Chuo cha Uongozi Mwl. Nyerere Kibaha, Pwani, tarehe 14 Januari, 2025.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Wizara ya Katiba na Sheria imeendelea
kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria kupitia
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) zinafikia Watanzania kwa
ufanisi. Katika hatua ya kuimarisha utekelezaji wa kampeni hiyo, mafunzo maalum
yametolewa kwa waratibu wa MSLAC kutoka maeneo mbalimbali nchini. Tarehe 14
Januari, 2025.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa
muda wa siku mbili katika Chuo cha Uongozi Mwl. Nyerere Kibaha, Pwani,
yamewalenga waratibu wa kampeni kwa lengo la kuwaongezea ujuzi na maarifa ya
jinsi ya kusimamia, kuratibu, na kufikisha huduma za msaada wa kisheria kwa
wananchi kwa ufanisi zaidi.
Comments
Post a Comment