4RS ZA RAIS SAMIA ZAITIKISA GENEVA
Akizungumza wakati
akiiwakilisha Nchi ya Tanzania katika Kikao cha 58 Cha Haki za Binadamu
kinachofanyika Geneva Nchini Uswisi tarehe 24 Februari, 2025 Waziri wa Katiba
na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa, Nchi ya
Tanzania imeendelea kuweka kipaumbele katika uendelezaji na ulinzi wa Haki za
Binadamu katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.
Waziri Ndumbaro amesema
kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 na Katiba ya Zanzibar,
1984, Tanzania imeendelea kusimamia Utu wa Kibinadamu kwa mujibu wa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na Tamko la Kimataifa la Haki
za Binadamu na inaendana na mkakati uliopitishwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambao umejikita katika
4Rs kuwa ni Maridhiano, Uthabiti,Mageuzi na Kujenga upya.
Akiwasilisha taarifa kuhusu
utekelezaji wa Haki za Binadamu katika Hifadhi ya Ngorongoro, Waziri Ndumbaro
amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuweka uwiano sawa wa haki
za binadamu na maisha kwa kuzingatia uhifadhi.
Waziri Ndumbaro amefafanua
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimami haki za binadamu
Ngorongoro alikutana na Viongozi wa Vijiji na Kimila na kusikiliza kero zao na
kuanzisha Tume mbili za Ushauri, kushauri masuala ya Ardhi na kushauri kuhusu mpango
unaoendelea wa kuwahamisha wakazi wa Ngorongoro kwenda Msomera.
Aidha, Waziri Ndumbaro
ameongezea lengo la jitihada hizo ni kuhakikisha zoezi la hiari linafanya kazi
kwa urahisi na kwamba kero za wananchi zinashughulikiwa.
Comments
Post a Comment