KASI YA ELIMU YA KUANDIKA NA KUTUNZA WOSIA IONGEZWE
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria
kuongeza kasi katika kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuandika na kutunza wosia
pamoja na kugawa mirathi kwa mujibu wa sheria ili kupunguza migogoro ya kijamii
nchini.
Wakati akizindua kampeni ya
Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoani Lindi, Waziri Mkuu pia
amewaagiza wakuu wa wilaya kote nchini kuwatumia Mawakili wa serikali ngazi ya
Wilaya, Halmashauri na Mikoa katika kuwa na programu mbalimbali za kusikiliza
na kutatua kero za kisheria kwa wananchi ngazi ya Halamshauri.
Wakati wa hotuba yake Waziri
Mkuu pia amewahimiza Viongozi wa dini na Viongozi wa kimila kuendelea kuhubiri
na kuhimiza kuhusu upendo, Mshikamano na maadili mema kuanzia ngazi ya familia
ili kuendelea kutunza amani, umoja na mshikamano wa jamii.
Waziri Mkuu Majaliwa ametumia
fursa hiyo pia kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa maamuzi yake ya kuanzisha na kugharamia kampeni ya msaada wa
Kisheria ya Mama Samia ambayo kufikia mwezi Mei mwaka huu kampeni hiyo itakuwa
imefanyika kwenye mikoa yote ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibara ikiwa na
lengo la kusaidia jamii dhidi ya changamoto mbalimbali za
kisheria bila ya gharama.
Comments
Post a Comment