MSLAC IMESAIDIA KUKUZA UELEWA WA KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KWA WANANCHI NA WATENDAJI
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Abdalah Sagini amesema Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa
Kisheria ya Mama Samia imesaidia kukuza uelewa wa kisheria na haki za binadamu
kwa wananchi na watendaji wa serikali huku pia ikikuza na kuimarisha huduma za
ushauri wa kisheria na unasihi kwa waathirika wa vitendo mbalimbali ya
kikatili.
Mhe. Sagini amebainisha hayo Februari
19, 2025 wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Lindi, akisema pia kampeni
hiyo imesaidia kukuza imani kwa wananchi katika utatuzi wa migogoro mbalimbali
kwa njia mbadala sambamba na kukuza uelewa wa watendaji wa serikali ngazi ya
jamii kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo sheria, utawala bora na utawala wa
sheria kama nguzo kuu ya maendeleo, amani na utulivu wa nchi.
Comments
Post a Comment