MSLAC INATEKELEZA FALSAFA YA 4R ZA RAIS SAMIA
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ameitaja Kampeni ya kitaifa ya
msaada wa Kisheria ya Mama Samia kuwa ya kipekee, mahususi na inayotekeleza
sharti la kisheria la kuwa na msaada wa kisheria kwa wananchi na yenye
kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya 4R yenye
kuhimiza kuhusu maridhiano na ujenzi wa Tanzania mpya.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni
hiyo mjini Ruangwa mkoani Lindi mbele ya Mgeni Rasmi Mhe. Kassim Majaliwa,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Kabudi amesema kwa
Tanzania sharti la msaada wa kisheria limepanua wigo zaidi kwani linatoa msaada
kwenye kesi zote ikiwemo zile za madai pamoja na jinai.
Prof. Kabudi ameitaja
wizara ya Katiba na Sheria kuwa mtekelezaji mkubwa na msimamizi wa falsafa hiyo
ya Rais Samia Suluhu Hassan, akimshukuru pia kwa kuasisi kampeni hiyo pamoja na
uwezeshaji wake mkubwa alioutoa kuwezesha kampeni hiyo kuwafikia watu wengi
zaidi hasa wale wa maeneo ya pembezoni na wasiokuwa na
uwezo wa kiuchumi.
Comments
Post a Comment