TUMIENI SAMIA LEGAL AID KUTOA HAKI - RC MTANDA

 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda akikagua banda la Wizara ya Katiba na Sheria alipowasili katika viwanja vya Furahisha kabla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Februari 18, 2025.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Alfred Dede akitoa salamu za Wizara kwa Niaba ya Katibu Mkuu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Februari 18, 2025 Jijini Mwanza.

Wananchi wa Mkoa wa Mwanza wakiwa  katika maandamano kuelekea katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ikiwa ni Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya  Mama Samia Legal Aid tarehe 18 Februari,  2025 katika Viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewasihi viongozi wa Mkoa huo kuendelea kutoa haki kwa wananchi bila upendeleo ili kuwaletea wananchi hao Maendeleo.

Mhe. Mtanda amesema hayo Februari 18, 2025 Jijini Mwanza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign).

Kampeni hiyo itakuwepo Jijini Mwanza kwa siku 9 baada ya Uzinduzi ambapo Jopo la wataalamu wa sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria litakua likitoa huduma hiyo katika Halmashauri zote za Jiji la Mwanza.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Alfred Dede akitoa salamu za Wizara kwa Niaba ya Katibu Mkuu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Februari 18, 2025 Jijini Mwanza.



Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA