WANASHERIA WA SAMIA WAMALIZA MGOGORO WA MAJIRANI MWANZA
Jopo la Wanasheria wa Serikali
kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Haki za
Binadamu Bi. Beatrice Mpembo Februari 19, 2025 Jijini Mwanza wamefanikiwa
kutatua changamoto ya ardhi iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kata ya
Nyamagana.
Hayo ya yamejili kufuatia
utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal
Aid Campaign) Jijini humo ambapo majirani hao Johanes Johnbosco na Bw. Yassin
Suleiman walitofautiana kwenye matumizi ya ardhi.
Imeelezwa kwamba Bw. Johanes
aliingia makubaliano ya kuchimba na kujenga shimo la maji taka katika eneo la jirani
yake huyo kupitia kwa mmiliki wa awali wa eneo hilo baada ya Bw. Johanes
kukumbana na changamoto ya mwamba katika eneo lake.
Hata hivyo shimo hilo limekuwa
likitumiwa kwa pamoja na mmiliki wa awali hadi mmiliki wa sasa kabla ya
kupishana na kumtaka Bw. Johanes kuacha kutumia shimo hilo
Baada ya wanasheria hao kufika
eneo la tukio wamefikia maridhiano kuwa kwa sasa waendelee kutumia pamoja huku
Bw. Yassin akitoa kipande cha ardhi yake kumpatia Johanes ili ndani ya miaka
mitatu ajenge shimo lake katika kipande hicho.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria
ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid) inaendelea katika Halmashauri zote nane za
Jiji la Mwanza ambapo wataalamu wa Sheria wanaendelea kutoa elimu na kutatua
migogoro mbalimbali.
Comments
Post a Comment