KAMATI ZA USALAMA ARUSHA ZATAKIWA KUFANYA KAZI KAMA TIMU
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Paul Christian Makonda, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya
Usalama Mkoa, Wawezeshaji wa Mafunzo ya
Utawala Bora na Urai mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya Uraia na Utawala Bora
mafunzo yanayoratibiwa na Wizara ya
Katiba na Sheria kupitia Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki. Tarehe 13
Machi, 2025.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Paul
Makonda, amewataka wajumbe wa Kamati za Usalama mkoani humo kufanya kazi kama
timu, pamoja na kuwa na vipaumbele vya miradi ya kimkakati inayopaswa kujivunia
kwa viongozi wa kitaifa wanapotembelea mkoa huo.
Makonda amezungumza hayo
wakati akifunga mafunzo ya elimu ya uraia na utawala bora kwa wajumbe wa Kamati
ya Usalama wa Mkoa wa Arusha pamoja na kamati za usalama za Wilaya ya Arusha na
Arumeru, yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria, tarehe 13 Machi, 2025.
Amesema Arusha kama mkoa
unapaswa kuwa na mambo makubwa yanayoweza kufanywa kipaumbele kwa viongozi wa
Kitaifa hususan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan, hivyo ni muhimu kamati za usalama kutambua kila mradi unaotekelezwa na
ukubwa kishwa kuainisha ile yenye kuuzika kwa wananchi na viongozi wakuu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango
na Bajeti wa Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kwambaza, ameeleza lengo la
kutoa mafunzo hayo kuwa ni pamoja na “kuboresha utendaji kazi wa viongozi wa Serikali
za Mitaa kwa kuzingatia haki za binadamu, utawala bora, demokrasia na kudumisha
ulinzi na usalama.”
Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Elisante Ulomi, mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi, amesema moja ya mambo muhimu ya Kamati za Usalama Arusha kupata mafunzo
hayo na kufundishwa kuhusu Ulinzi na Usalama, ni kutokana na mkoa huo kuwa wa
kimkakati pamoja na miradi mikubwa inayotekelezwa yenye masilahi makubwa kwa
taifa ukiwamo Uwanja wa Mpira.
“Ni mkoa ambao una vivutio
vingi vya utalii lakini pia una watalii wengi ambao wanatoka nje ya nchi kuja
Arusha.” Amesema ACP Ulomi.
Mratibu wa mafunzo hayo kutoka
Wizra ya Katina na Sheria Wakili wa Serikali Mkuu Bi. Joyce Mushi, amesema
“katika mafunzo mada mbalimbali zimetolewa na mada kubwa ambayo imewahusu washiriki
hawa ni mada ya ulinzi na usalama, washiriki wamepokea mafunzo haya na
wameahidi kwamba watakwenda kuyafanyia kazi kwasababu ni mafunzo ambayo
yanawagusa moja kwa moja.”
Comments
Post a Comment