Mama
Samia Legal Aid Campaign Yaweka Kambi Arusha.
Timu ya watoa Huduma za Msaada
wa Kisheria kupitia Kampeni ya "Mama Samia Legal Aid" imeweka kambi
rasmi Machi 27, 2025 Jijini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa kuihudumia Jamii
inayokabiliwa na uhitaji wa Msaada wa Kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Paul Christian Makonda amewashauri watumishi wa Samia Legal Aid kuwa wasikivu
na kutanguliza utu wanaposhughulikia kero za Wananchi, kwani wanamwakilisha
Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye shauku yake kubwa ni Wananchi kutatuliwa changamoto
zao.
"Mnatakiwa kuwa wasikivu
na kutanguliza utu mnaposhughulikia kero za wananchi, kwani mnamwakilisha Rais
Samia Suluhu Hassan, ambaye shauku yake kubwa ni wananchi kutatuliwa changamoto
zao."
Mhe. Makonda amesema hayo
wakati akiongea na wataalam wa Sheria wakiwemo mawakili, maofisa maendeleo ya
jamii pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali waliokutana kwaaajili ya
kupanga mikakati ya utatuzi wa changamoto za wananchi katika Halmashauri saba
za Mkoa wa Arusha pamoja na kuainisha changamoto zinazopaswa kufanyiwa kazi
katika kila idara husika.
“Tunatofautiana katika
kujielezea. Jipe muda, rudia tena, muulize mtu maswali vizuri ili tupate ukweli
na tuweze kumaliza matatizo ya wananchi. Lakini, toeni maamuzi,” amesema Makonda.
Aidha, ametoa wito kwa
Wananchi wa Arusha kufika katika viwanja vya Ngarenaro siku ya kesho machi 28
ili kupata haki yao.
Timu ya Wanasheria itakuwa mkoani Arusha kwa siku 9 kwa ajili ya kusikiliza na kutatua migogoro ya kisheria kwa Wananchi wa Wilaya zote za Mkoa wa Arusha.
Comments
Post a Comment