MASWI AHIMIZA KUKAMILISHWA UJENZI WA JENGO LA WIZARA MTUMBA
Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi alipotembelea na kukagua
maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma.
Tarehe 11 Machi, 2025.
xxxxxxxxxxxxxxxxx
Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi amesema kuwa Wizara itaanza
matumizi ya ofisi za jengo jipya ambalo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi
wake kwa kuhakikisha yeye mwenyewe akiwa ameambatana na timu ya Menejimenti
inaanza kutumia jengo hilo ambalo mpaka sasa limefikia asilimia 86 ya ujenzi.
Katibu
Mkuu Maswi amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa
jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma Machi 11, 2025 huku akimhimiza
Mkandarasi SUMA JKT Kanda ya Mashariki kuongeza kasi zaidi ili kuendana na
makubaliano ya mkataba wa ukamilishaji wa jengo hilo.
"katika
kuendelea kuboresha utendaji kazi wa Wizara tumefanikiwa kupata Watumishi wapya
na wapo Watumishi waliohamia hivyo uhitaji wa ofisi ni mkubwa sana. Nimeona ni
vyema nianze mimi kuhamia nafikiri nikifanya hivyo kazi itakwenda kwa kasi mimi
nipo tayari na kuanzia tarehe 17 Machi, 2025 kazi zangu zitakuwa katika jengo
jipya" alisema Maswi.
Kukamilika
kwa jengo hilo jipya kunataraji kuboresha mazingira ya utoaji Huduma
za Wizara na kuwezesha mazingira bora ya kazi kwa Watumishi.
Comments
Post a Comment