OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA MWANZA YAHIMIZWA UWAJIBIKAJI
Waziri wa Katiba na Sheria,
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Machi 18, 2025 Jijini Mwanza ameongoza kikao na watumishi wa Ofisi ya
Mwendesha Mashtaka wa Mkoa huo ambapo
amewahimiza umuhimu wa uwajibikaji katika kazi zao.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Ndumbaro amesisitiza kwamba
ni muhimu kwa watumishi hao kuongeza ufanisi ili kuboresha huduma wanazotoa kwa
wananchi na kusaidia katika utoaji wa
Haki kwa wananchi.
Nae Mkuu wa Mashtaka wa Mkoa
huo Bw. Joseph Mahugo, amemthibitishia Waziri Ndumbaro kwamba ofisi yake
itaendelea kutoa huduma bora kwa maslahi ya taifa.
Ziara ya Waziri Ndumbaro
Jijini Mwanza ina lengo la kufanya ukaguzi wa shughuli za ofisi hiyo na kuona
jinsi wanavyoweza kuboresha huduma zao kwa umma.
Comments
Post a Comment