SIMAMIENI MALALAMIKO YA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU - DKT. MWANDAMBO
Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Jiji la Tanga Dkt. Stephen Mwandambo amewataka Watendaji wa Kata
kusimamia malalamiko ya wananchi ya ukiukwaji wa Haki za Binadamu.
Dkt. Mwandambo ameyasema hayo tarehe
15 Machi, 2025 wakati akifungua mafunzo ya Uraia na Utawala Bora kwa Kamati ya
Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watendaji wa Kata wa Halmashauri ya Jiji
la Tanga.
“Mafunzo haya yatamsaidia
Mkurugenzi kutoa nafuu kwenye utekelezaji wa
majukumu na tunategemea kuona
huduma zimeboreshwa katika ngazi zote baada ya mafunzo haya.“
Mwandambo amesema kupitia
mafunzo waliyopata watatekeleza kwa vitendo na kuhakikisha falsafa ya “4R“ ya
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inasambaa kutoka katika ngazi za chini mpaka za
juu za uongozi.
Awali Wakili wa Serikali
Kutoka Wizara ya katiba na Sheria na Mratibu wa Mafunzo Adv. Dorice Dario
ameeleza malengo ya mafunzo hayo ni kuwawezesha Viongozi wa Serikali za Mitaa
kuongeza ujuzi na maarifa yatakayo wasaidia kupokea na kushughulikia malalamiko
ya wananchi yanayofikishwa mezani kwao.
Comments
Post a Comment