WATENDAJI WA KATA KUWENI WAZALENDO KWA MASLAHI YA TAIFA
Watendaji wa kata wa Wilaya ya
Mkinga wametakiwa kuwa wazalendo kwa kuacha tabia ya kuwasaidia raia wa kigeni
kupata vitambulisho bila kufuata taratibu za nchi kwa kuwa kufanya hivyo ni
hatari kwa mustakabali wa Taifa.
Rai hiyo imetolewa na Afisa
Tawala Mwandamizi Erick Farahani wakati alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya
Mkinga Mhe. Gilrbet Karima katika kufungua Mafunzo ya Uraia na Utawala Bora kwa
Kamati ya Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Watendaji wa Kata yanayoratibiwa na
Wizara ya Katiba na Sheria.
“Sisi ndio tunaohusika kuwatambulisha
wananchi, hii imekuwa ni changamoto kwetu sisi mpakani, mnapomtambulishi mtu
kana kwamba yeye ana haki za uraia wa Tanzania tunawaomba kuwa wazalendo kweli”
Kwa upande wake Wakili wa Serikali
kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Adv. Dorice Dario amesema malengo ya kutoa
elimu hiyo ni kuboresha utendaji kazi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa
kuzingatia haki za binadamu na utawala bora.
Comments
Post a Comment