WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ZINGATIENI SHERIA - KM MASWI
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg.Eliakim Maswi
akizungumza na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali na Mtandao wa Watetezi
wa Haki za Binadamu (THRDC)ambapo ametoa wito kwa wadau hao kuzingatia Sheria
za Nchi na kufanya kazi kwa ushirikiano
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Katiba na Sheria, Ndg. Eliakim Maswi ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya
kiserikali pamoja na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)
kuhakikisha wanafuata sheria za nchi, taratibu zilizowekwa, na kufanya kazi kwa
ushirikiano bila ubinafsi.
Maswi ametoa wito huo Machi
18, 2025 jijini Dodoma, wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa wanachama
wapya wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC.)
Amesema kuwa mashirika hayo
yana nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo juu ya sheria zinazowasimamia, ili
serikali iweze kufanya mabadiliko pale inapohitajika kwa ajili ya kuimarisha
haki za binadamu kwa wananchi.
Aidha, amewataka wanachama
wapya wa THRDC kuwa mabalozi wa haki za binadamu katika maeneo wanayotoka, kwa
kuhakikisha wanachochea mabadiliko chanya kwenye jamii zao.
Kwa upande wake, Mratibu wa
THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema kuwa ukiukwaji wa haki za watoto umekuwa
changamoto kubwa inayozidi kukithiri nchini jambo ambalo
wanapaswa kuongeza nguvu katika kukabiliana nalo.
Comments
Post a Comment