UZINDUZI WA MSLAC KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Mwassa akiwasili katika Uwanja wa Uhuru (Mashujaa) Mkoani Kagera kwa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia leo Aprili 14, 2025. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Uhuru (Mashujaa) Mkoani Kagera kwa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia leo Aprili 14, 2025. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Jasson Rwezimula akitoa Salaam za Wizara wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Kagera. Tarehe 14 Aprili, 2025. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Kagera tarehe 14 Aprili, 2025