Monday, May 18, 2020

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKUTANA NA WAKILI MKUU WA SERIKALI

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba afanya mazungumzo na Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Clement Mashamba ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na mgeni wake Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Clement Mashamba (wa pili kulia) baada ya kumtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Thursday, May 14, 2020

KIKOSI KAZI KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WAFUGAJI NCHINI KUUNDWA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiongoza kikao cha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Makatibu Wakuu wa Wizara za  Katiba na Sheria, Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii na Mwendesha Mashtaka nchini kujadili suluhisho la malalamiko ya wafugaji.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (aliyenyanyua mkono) akifafanua jambo katika kikao cha viongozi kujadili suluhisho la malalamiko ya wafugaji.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiongea  katika kikao cha viongozi kujadili suluhisho la malalamiko ya wafugaji.

Tuesday, May 12, 2020

MWENYEKITI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA AMTEMBELEA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea makabrasha yanayohusu majukumu ya Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe.  Jaji Mstaafu Januari Msoffe alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kwa Waziri baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.

Mhe.  Jaji Mstaafu Januari Msoffe (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba  alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha. Mwingine kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma wizarani hapo Bw. Griffin Mwakapeje.


 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba  akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe.  Jaji Mstaafu Januari Msoffe na ujumbe wake walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha.


Monday, May 4, 2020

MWIGULU ATAKA HAKI ZA BINADAMU ZILINDWE

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akipokea maua kutoka kwa Wakili wa Serikali Bi. Esther Msambazi alipofika kwa mara ya kwanza Wizarani hapo baada ya kuapishwa jana kuiongoza wizara hiyo.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akiwa Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma kwa mara ya kwanza, baada ya kuapishwa jana kuiongoza wizara hiyo.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akiwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi katika kikao kifupi cha ukaribisho aliporipoti ofisini kwake leo (Mei 04/2020) Mtumba, jijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akiwaongoza watumishi wa Wizara hiyo kumuombea mtangulizi wake aliyefariki hivi karibuni.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXWaziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amesema atasimamia yale ambayo ana hakika ni matamanio ya  Rais Magufuli kuona yakitekelezwa kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ikiwemo kuona haki za binadamu hazipotei.

Akizungumza leo Mei 4, 2020 aliporipoti  ofisini kwake baada ya kuteuliwa na Rais kushika wadhifa huo na kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo katika kikao kifupi cha ukaribisho Waziri Nchemba amesema  “Tupo kwenye Wizara ambayo ipo kwenye maeneo ambapo nna hakika Rais ameandika moyoni mwake kuona yakilindwa ikiwemo kuona haki za binadamu hazipotei”

Amesema, ni lazima katika majukumu ya Idara na Vitengo vyetu tulipe  kipaumbele suala hili na kuhakikisha linafanikiwa.

Mbali na kutaka upatikanaji wa haki za binadamu uzingatiwe Waziri Nchemba alisisitiza watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili kuleta matokeo yanayotarajiwa na Rais na pia kulinda rasilimali zilizopo.

Waziri Nchemba aliwaomba watumishi kuendeleza ushirikiano uliokuwepo tangu enzi za mtangulizi wake na kuchapa kazi kwa juhudi zote. Pia aliwataka kuangalia maeneo mapya na kuibua fursa mbalimbali zitakazoleta tija katika Wizara hiyo.

Aidha, awali akimkaribisha Waziri Nchemba, Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome alimueleza Waziri huyo kuwa  watumishi wapo tayari kushirikiana nae na kuunga mkono juhudi za Rais za kuliletea maendeleo Taifa letu.