Posts

Showing posts from January, 2024

BALOZI DKT. CHANA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea kwenye kikao na Balozi wa Uingereza, tarehe 31 Januari, 2024 Ofisi za Bunge, Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea kwenye kikao na Balozi wa Uingereza, tarehe 31 Januari, 2024 Ofisi za Bunge, Dodoma. Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Balozi David Concar akiongea kwenye kikao na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi, tarehe 31 Januari, 2024 Ofisi za Bunge, Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar, tarehe 31 Januari, 2024 Ofisi za Bunge, Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar, kwenye picha ya pamoja na walishiriki katika kikao hicho, tarehe 31 Januari, 2024 Ofisi za Bunge, Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufany

TUKO VIZURI KWENYE SUALA LA AMANI – DKT. CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na Wanahabari kwenye Viwanja vya Nyerere Square, 30 Januari, 2024 Wakili wa Serikali Mkuu Bw. Emmanuel Mbega akitoa maelezo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipotembelea banda la Wizara, tarehe 30 Januari, 2024 Viwanja vya Nyerere Square. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akipata maelezo alipotembelea Banda wa Wadau wa Haki Jinai, tarehe 30 Januari, 2024 Viwanja vya Nyerere Square. Bw. Laurent Burilo akipokea Cheti cha Ushiriki wa Wizara kwenye Maonesho ya Madhimisho ya Wiki ya Sheria kutoka kwa Kaimu Msajili wa Mahakama Mhe. Sylvester Kainda, tarehe 30 Januari, 2024 Viwanja vya Nyerere Square. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema dunia ina imani na amani iliyoko nchini amani ambayo inachagizwa na utawala wa sheria. Dkt. Chana amesema hayo alipotembelea mabanda ya maoenesho k

SERIKALI YABORESHA HUDUMA ZA HAKI JINAI KWA NJIA YA TEHAMA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi kutoka kwenye taasisi zilizo chini ya Wizara baada ya kikao cha makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA kilichofanyika mtumba leo tarehe 30 Januari 2024 Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana akikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Mkuu wa Gereza la Msalato Ndg Flavian Justin wakati wa makabidhiano yaliyofanyika leo tarehe 30 Januari 2024 Jijini Dodoma.  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana akiongea Jambo kwenye kikao cha makabidhiano ya Vifaa vya TEHAMA kwa baadhi ya Taasisi zilizo chini ya wizara kilichofanyika leo tarehe 30 Januari 2024, Jijini Dodoma  X XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku - WKS Dodoma.   Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeendelea kuonesha nia yake thabiti ya kuboresha upatikanaji haki kwa wakati kwa  kutoa vifaa vya TEHAMA vitakavyorahisisha huduma za Haki katika taasisi mbalimbali zinazohus

WAZIRI CHANA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI WA UNICEF TANZANIA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Balozi Pindi Chana akifafanua jambo wakati wa kikao na Mwakilishi Mkuu wa UNICEF nchini Bi, Elke Wisch kilichofanyika leo tarehe 30 Januari 2024 jijini Dodoma.    Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Balozi Pindi Chana akipeana mikono na mwakilisha mkuu wa shirika la UNICEF nchini Bi, Elke Wisch baada ya kikao kilichofanyika leo tarehe 30 Januari 2024 Jijini Dodoma.      Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Balozi Pindi Chana akiwa kwenye picha ya  pamoja na Mwakilishi Mkuu wa UNICEF nchini Bi, Elke Wisch baada ya kikao kilichofanyika leo tarehe 30 Januari 2024 Jijini Dodoma.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George Mwakyembe -   WKS Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkuu wa Shirika la kuhudumia watoto nchini (UNICEF) Bi, Elke Wisch na kujadili masuala mbalimbali kuhusu haki za watoto. Katika kikao hicho ambacho kimefanyika leo tarehe 30 Janu

WAZIRI CHANA AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA TAASISI YA USULUHISHI TANZANIA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya usuruhishi nchi(Tanzania Institute of Arbitrators ) pamoja na Watumishi wa Wizara  kwenye kikao kilichofanyika leo tarehe 29 Janauri 2024 jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana akitoa ufafanuzi kwenye  kikiao na viongozi wa Taasisi ya usuruhishi (Tanzania Institute of   Arbitrators) kilichofanyika leo tarehe 29 Janauri 2024 jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana akipokea vitabu kutoka kwa Makamu wa Rais wa Taasisi  ya Usuruhishi Ndg, Anderickson Njunwa kwenye kikiao kilichofanyika leo tarehe 29 Janauri 2024 jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George Mwakyembe - WKS Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya kikao na viongozi kutoka Taasisi ya Usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara kwa Njia Mbadala - TIARB (Tanzania Insitute of Arbitrators) na kujadili masuala mbalimbal

SERIKALI KUANZISHA KITUO CHA KUDUMU KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO

Image
Wakili wa Serikali Bi. Agness Mkawe kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akitoa maelezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi alipotembelea banda la Wizara, kwenye viwanja vya Nyerere Square, tarehe 28 Januari, 2024. XXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amesema Serikali inaangalia uwezekano wa kuanzisha kituo cha kudumu Makao Makuu ya nchi kushughulikia kero za wananchi. Dkt. Feleshi ameyasema hayo alipoongea na Wanahabari baada ya kutembelea mabanda kwenye viwanja vya Nyerere Square kunakofanyika maonesho ya Wiki ya Sheria tarehe 28 Januari, 2024. “Pamoja na maadhimisho ya Wiki ya Sheria kila mwaka, matumizi ya kurasa za maoni kwenye tovuti, simu za kupokelea maoni na sasa kuna Mama Samia Legal Aid Campaign ambayo hadi sasa imetekelezwa kwenye mikoa sita Tazania Bara tungeweza kusema sasa mifumo ya kupokelea maoni na malalamiko inatosha, lakini unaona malalamiko yapo, bado wananchi wan

MAHAKAMA IJIANDAE KUKABILIANA NA WIMBI LA KESI ZA AKILI BANDIA (ARTIFICIAL INTELLIGENCE)

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akihutubia kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma tarehe 27 Januari, 2024 Bw. Emmanuel Mbega Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akitoa maelezo kwa Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwenye Banda la Wizara, tarehe 27 Januari, 2024 kwenye Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Dkt. Tulia Ackson ameitaka Mahakama ya Tanzania kujiandaa kukabiliana na waathirika wa matumizi ya akili bandia wakati ikiendelea kuboresha matumizi ya TEHAMA katika kutoa haki. Dkt. Tulia ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma tarehe 27 Januari, 2024 ambapo yeye alikuwa Mgeni Rasmi. Kabla ya uzinduzi huo Dkt. Tulia aliongoza matembezi yaliyoanzia Kituo Jumuishi cha Ut

CHETI CHA KUZALIWA SIO KIGEZO PEKEE CHA URAIA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na Watendaji wa Ofisi ya RITA ya Njombe, 27 Januari, 2024 Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Ofisi ya RITA Njombe Mjini, 27 Januari, 2024.                                XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX  Na Lusajo Mwakabuku - Njombe Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema cheti cha kuzaliwa hakimpi mtu yeyote uhalali wa uraia wake bali ni uthibitisho wa kuzaliwa kwake au kinaweza kutumika kama moja ya kigezo cha kuthibitisha uraia. Waziri Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati alipotembelea Ofisi za Msajili wa Vizazi na Vifo Mkoa wa Njombe kwa lengo la kuangalia hali uandikishaji usajili wa watoto chini ya miaka mitano, tarehe 27 Januari, 2024. “Sio uthibitisho pekee na ndiyo maana cheti cha kuzaliwa hata mtoto ambaye wazazi wake wote wawili sio watanzania ni wageni wamekuja kutalii akizaliwa Tanzania atapata cheti hivyo katik

WAZIRI CHANA AFANYA KIKAO CHA KIMKAKATI NA MENEJIMENTI YA WIZARA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea kwenye kikao na Menejimenti ya Wizara kilichofanyika Mtumba leo tarehe 24 Januari, 2024 jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana akiwa kwenye kikao na Menejimenti ya Wizara kilichofanyika Mtumba leo tarehe 24 Januari 2024 jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George Mwakyembe – WKS Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.   Balozi Dkt. Pindi Chana amefanya kikao na Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 24 Januari, 2024 katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma kikiwa na malengo ya kutathmini kwa kina utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa nusu muhura wa bajeti ya mwaka 2023/ 2024. Mhe. Waziri Chana ameiopongeza Menejimenti na watumishi wote kwa ujumla kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuhakikisha kazi za kuwahudumia wanachi zinakwenda vizuri na kwa wakati.

MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA YAANZA VIWANJA VYA NYERERE DODOMA

Image
  Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe. Dkt. Juliana Masabo akisaini kitabu cha mahudhurio kwenye Banda la Wizara kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria, tarehe 24 Januari, 2024 viwanja vya Nyerere Square XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Madhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo huandaliwa na Mahakama ya Tanzania kila mwaka yameanza leo tarehe 24 Januari, 2024 kwenye viwanja vya Nyerere Square, Jijini Dodoma ambapo Wizara ya Katiba na Sheria inashiriki. Maadhimisho hayo ya siku tisa yaliyobeba kauli mbiu ”Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai” yatazinduliwa rasmi tarehe 27 Januari, 2024 na kufungwa rasmi tarehe 1 Februari, 2024. Wakati wote wa maadhimisho hayo Wizara itakuwa inatoa elimu ya sheria na huduma ya msaada wa kisheria.    

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MAJIBU YA SERIKALI

Image
Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akichangia kujibu hoja kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Wizara, tarehe 23 Januari, 2024 Kumbi za Bunge. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo (kushoto), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) wakifuatilia kwa makini majibu ya Serikali kuhusu hoja za Bunge, tarehe 23 Januari, 2024 Kumbi za Bunge. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi - WKS Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Florent Kyombo imeridhishwa na majibu ya hoja zote kumi zilizowasilishwa na Bunge kwa Wizara ya Katiba na Sheria mwezi Februari, 2023. Kikao cha Kamati hiyo kimefanyika tarehe 23 Januari, 2024 kwenye kumbi za Bunge ambapo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongozana na Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Mary Makondo, baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Wataala

DKT CHANA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI MAJUKUMU YA WIZARA KWENYE KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Pindi Chana akifuatilia ufafanuzi ulikuwa unatolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na sheria leo tarehe 22 Januari 2024 Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana akitoa ufafunuzi kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge, utawala katiba na sheria leo tarehe 22 januari 2024 Jijini Dodoma.  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Balozi Pindi Chana akijadili jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt Eliezer Feleshi kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge, utawala katiba na sheria leo tarehe 22 Januari 2024 Jijini Dodoma. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge, utawala Katiba na sheria wasikiliza uwasilishwaji wa maada wakati wa kikao leo tarehe 22 Januari 2024 Jijini Dodoma.   XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe - WKS Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana amewasilisha taarifa ya utakelezaji   wa majukumu ya Wizara kwenye Kam

TUTAENDELEA KUTOA ELIMU NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KISHERIA KWA WANANCHI

Image
Katibu Tawala wa Wilaya Singida Bi. Naima Bakari Chondo, akiongea baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa MSLAC katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, tarehe 19 Januari, 2024. Bi. Basuta Milanzi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa MSLAC katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwa Katibu Tawala wa Wilaya Singida Bi. Naima Bakari Chondo, tarehe 19 Januari, 2024 XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Singida Katibu Tawala wa Wilaya Singida Bi. Naima Bakari Chondo ameahidi kutekeleza changamoto za wananchi ambazo hazikutatuliwa katika kipindi cha kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ili kuendelea kutatua migogoro kwenye jamii. Bi. Naima ametoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Kampeni hiyo iliyokuwa inafanyika kwenye Halmashauri yake kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, tarehe 19 Januari, 2024. Aidha, akiongelea changamoto za kesi za ukatili wa kijinsia amesema, “ipo changamoto ya kesi za ukatili wa kijinsia na kuzifanya kuwa ngumu kuendesha na

TUWASHIRIKISHE WANANCHI ULINZI WA UTAJIRI ASILIA

Image
  Mgeni Rasmi Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali waliofika katika mafunzo hayo ya kujengeana uwezo juu ya mali asilia, Januari 18, 2024 Jijini  Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana akizungumza na Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utajiri na Mali Asili za nchi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa majadiliano, Januari 18, 2024 Jijini Dar es salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Dr. Khatibu Kazungu akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa katiba na Sheria kutoa hotuba yake, Januari 18, 2024 Jijini Dar es Salaam. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku - WKS Dar es Salaam Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana amewataka Viongozi wa umma wenye jukumu la kusimamia Utajiri Asili na Mali Asilia za nchi kuwashirikisha wananchi katika kulinda rasilimali hizo ili kuhakikisha zinalinufaisha taifa na wananchi kwa uju

WANANCHI WASHAURIWA KUIBUA KERO NZITO NZITO KUITWISHA MSLAC

Image
  Afande Veronica Masele kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Halmashauri ya Wilaya ya Singida akitoa mada ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ikhanoda, 16 Januari, 2024. Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bi. Paskazia Kyaruzi akitoa mada kuhusu masuala ya ardhi, tarehe 16 Januari, 2024 Kijiji cha Ikhanoda. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Singida Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Ikhanoda Kata ya Ikhanoda katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bw. Jumanne Idabu amewataka wananchi kuibua kero ambazo zimeshindika na kuitwisha Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) ili zitatuliwe. Bw. Idabu alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kutekeleza kampeni hiyo uliofanyika kijijini hapo tarehe 16 Januari, 2024 ukihudhuriwa na wakazi wa vijiji vya Ikhanoda na Msimihi. “Wananchi ibueni kero nzito ambazo walau zimeshachukuliwa hatua katika ngazi mbalimbali bila mafanikio ili Kampeni hii itusaidie,” alisema.