Posts

Showing posts from April, 2023

Waziri Mkuu azindua Mama Samia Legal Aid Campaign Dodoma

Image
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), Bi. Rosemary Senyamule Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (kushoto) katika picha ya pamoja na sehemu ya Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwenye hafla ya uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign tarehe 27 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku - WKS   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameizundua rasmi kampeni ya msaada wa kisheria inayoitwa Mama Samia Legal Aid Campaign kwa mkoa wa Dodoma Aprili 27, 2023 huku akiwataka watanzania kuitumia kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kutoa taarifa kuhusu uwepo wa watu, au vikundi vya watu ambao ama wanajihusisha na ukatili wa kijinsia hususan kwa watoto.  Waziri Mkuu amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa sheria na upatikanaji haki, mifumo ya utoaji haki, masuala ya kisheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na taasisi za Serikali, Asasi za kiraia na Wadau wa Maendeleo katika utoaji huduma

Wizara ya Katiba na Sheria yafanya Kongamano la Kitaifa la Sheria ya Ndoa

Image
  Mgeni Rasmi kwenye Kongamano la Kitaifa la Sheria ya Ndoa, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walioshiriki kwenye kongamano hilo lililofanyika tarehe 26 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kimila walioshiriki kwenye kongamano hilo lililofanyika tarehe 26 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini walioshiriki kwenye kongamano hilo lililofanyika tarehe 26 Aprili, 2023 Jijini Dodoma.

Wizara ya Katiba na Sheria yawasilisha Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/24

Image
  Mhe. Dkt. Ndamas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, tarehe 25 Aprili, 2023 Bungeni Dodoma.

Ndumbaro awataka watumishi wa Serikali kuwa wabunifu.

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akihutubia kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, tarehe 24 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wawe wabunifu katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ili kuleta tija katika utendaji kazi. Mhe. Ndumbaro ameyasema hayo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, tarehe 24 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. “Fanyeni kazi kwa kujituma na kuwa wabunifu, miundo na mifumo iliyopo sasa ilibuniwa na watu na kila baada ya muda inatakiwa kufanyiwa mapitio na hilo litawezekana kama kuna ubunifu.” Alisema Dkt. Ndumbaro. Aidha, Dkt. Ndumbaro amewaasa wajumbe wa Baraza kutumia kikao hicho, kwanza kujadili utekelezaji wa mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha 2022/23 mafanikio, changamoto na ufumbuzi wake, pili kujadi

Ndumbaro afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akihutubia katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, tarehe 18 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Mwandishi wetu. Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Takwimu Jijini Dodoma tarehe 18 Aprili, 2023. Akifungua Mkutano huo wenye lengo la kuwapitisha watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Taarifa ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24 ya Ofisi hiyo ambapo watumishi watapata wasaa wa kuchambua vipaumbele vya mpango na bajeti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mwaka 2023/24 ili kuhakisha mafanikio yaliyofikiwa mwaka 2022/2023 yanaongezeka. Aidha, Mhe. Ndumbaro amewaasa watumishi wa Ofisi hiyo kuweka juhudi katika kutekeleza majukumu yao ili kulinda taswira ya jamii na kuwa chachu ya ma

Dkt. Ndumabro apokea Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Dkt. Damas Ndumbaro katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria na sehemu ya Menejimenti ya Wizara wakati wa hafla ya kupokea Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria, tarehe 11 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi - WKS   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Dkt. Damas Ndumbaro amepokea Taarifa za mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia Uchaguzi na Vyama vya Siasa Nchini na Mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia utoaji haki katika Mahakama za Mwanzo kutoka kwa Mhe. January H. Msoffe (Jaji Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Hafla hiyo imefanyika tarehe 11 Aprili, 2023 Ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma. Taarifa hizo zitawasilishwa Bungeni kwa mujibu wa sheria ili mchakato wa mabadiliko ya sheria hizo uanze. Katika hafla hiyo Dkt. Ndumbaro ametoa rai kwa Wizara na Taasisi zote za umma zinazotaka kufanya tafiti, marejeo au ubores

Mswada Sheria ya Ndoa Kuingia Bungeni

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na sehemu ya Menejimenti ya Wizara katika picha ya pamoja na Jukwaa la Wakurugenzi Wanawake walipotembelea ofisi za Wizara Mtumba, Jijini Dodoma Aprili 5, 2023. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx   Farida Khalfan & Lusajo Mwakabuku - WKS   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Jukwaa la Wakurugenzi Wanawake waliowakilisha mashirika takribani 400 yanayotetea haki za wanawake, wasichana na watoto nchini Tanzania, tarehe 05 Aprili, 2023 ofisini kwake, Mtumba Jijini Dodoma. Kupitia kikao hicho Waziri ameeleza nia ya Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka mswada wa mabadiliko ya Sheria ya Ndoa, 1971 katika Bunge hili la bajeti, ili kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini wa kuolewa na kuoa kama ilivyoelekezwa na Mahakama. Aidha, Wakurugenzi kutoka Jukwaa la Wakurugenzi Wanawake walitumia fursa hiyo kumhakikishia Waziri na ofisi yake ushirikiano katika kuhakikisha mchakato h

Waziri Ndumbaro Asisitiza Utafiti wa Kisheria Kabla ya Sheria Kutungwa

Image
  Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akihutubia katika Kongamano la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili ya Tanzania, lilioandaliwa na Tume ya kurekebisha sheria Tanzania,  tarehe 05 Aprili, 2023 Jijini Dodoma.                                                              xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx William Mabusi na Lusajo Mwakabuku - WKS Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesisitiza kufanya kwa utafiti wa kisheria kabla ya kutungwa kwa sheria ili sheria zitakazotungwa baada ya tafiti zitumike kwa muda mrefu kabla ya kufanyiwa marekebisho. Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo wakati alipofungua Kongamano la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili ya Tanzania, lilioandaliwa na Tume ya kurekebisha sheria Tanzania,  tarehe 05 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. “Kukosekana kwa utafiti wa kisheria hupelekea mabadiliko ya mara kwa mara ya sheria. Hivyo kabla ya sheria kutungwa utangulie utafiti wa kisheria. Sheria zikitungwa baada ya kufanyiwa u