Posts

Showing posts from February, 2023

UAPISHO WA NAIBU WAZIRI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Pauline Gekul kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023.   

HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA KUFIKA HADI VIJIJINI

Image
Waziri wa Ktiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akionyesha mkakati wa kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia baada ya kuzindua.  XXXXXXXXXXX Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar Kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo waungana kutekeleza kampeni ya Kitaifa ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayotekelezwa Kwa miaka mitatu kuanzia Februari 2023 hadi Februari 2026. Kampeni hii itaangalia zaidi upatikanaji haki kwa watu wasiojiweza hususan wanawake na watoto, haya yakiwa ni maagizo ya Rais kuwa kupata haki ni haki ya mwananchi. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizindua kampeni hiyo Leo Februari 15, 2023 katika hoteli ya Four Points jijini Dar Es Salaam. Dkt. Ndumbaro amesema Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar na Wadau wa Maendeleo kila mmoja alikuwa anatoa Huduma ya Msaada wa Kisheria kivyake lakini kuanzia sasa itafanyika kwa pamoja na kufikia ambapo hapakufikiwa mikoa yote Tanzania Bara na Zanzi

DKT. NDUMBARO AZINDUA KITABU CHA MIAKA 60 YA UHURU NA SEKTA YA SHERIA

Image
  XXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro amepongezwa kwa kusimamia ukamilishwaji wa uandishi na uchapishaji wa Kitabu cha miaka 60 ya Uhuru na Sekta ya Sheria tulipotoka,tulipo na tunapokwenda tangu mwaka (1961 - 2021). Kitabu hicho kimeweka historia na kumbukumbu  ya miaka 60 kinatoa kipimo tosha  cha maendeleo  katika taasisi mbalimbali za serikali kwa miongo yote 6 tangu uhuru ikiwa ni umri wa mtumishi wa Serikali kustaafu. Akitoa pongezi hizo wakati wa zoezi la Uzinduzi wa kitabu hicho leo Februari 7,2023 jijini Dodoma,aliyewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria katika Serikali ya awamu ya tano na  sasa Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi  amesema kuwa historia sio habari ya mambo yaliyopitwa bali ni mambo yaliyopita ambayo yanamwangwi kwa mambo yaliyopo kwa sasa. "Historia ni habari iliyopita ambayo yanaakisi mambo ya sasa ni chemichemi ambayo jamii iliyaishi,inayaishi na kurithisha kwa vizazi na vizazi kwa kuwekwa katika vitabu,