Posts

Showing posts from August, 2023

MAHAKAMA KUENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI – MHE GEKUL

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akijibu maswali bungeni leo tarehe 30 Agosti 2023 . Dodoma. Na. George Mwakyembe - WKS DODOMA.       Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ameeleza kuwa Mahakama inaendelea na mpango wa kujenga ofisi za Mahakama nchini kote na kwamba hadi sasa ofisi 18 za Mahakama za Wilaya zimeshajengwa na Mahakama za Mwanzo ni 71. Mahakama hizi zinajengwa kwa utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 Mhe. Gekul ameyasema hayo leo tarehe 30 Agosti 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini Mhe, Daimu Idd Mpakate ambaye aliuliza lini Mahakama itajenga Mahakama za mwanzo katika Tarafa ya Nalasi, Lukumbule, pamoja na Tarafa ya Namasakata. Pia, Mhe. Gekul amefafanua kuwa tayari Mahakama ya mwanzo ya Nalasi inajengwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa ni sehemu ya ujenzi wa mahakama 71 za mwazo ambazo zitajengwa nchi nzima na tayari mshauri elekezi ameanza kazi na ujenzi utaanza Oktoba 2023. Vilevile,

DKT NDUMBARO AFUNGUA KIKAO CHA MAJADILIANO CHA MCHAKATO WA WA KATIBA MPYA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damasi Ndumbaro   akiongea kwenye kikao cha Majadiliano ya   Katiba mpya   na Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba    kilichofanyika kwenye ukumbi Hyatt    Regency   leo tarehe 28 Agosti Jijini Dar es Salaam . Katibu Mkuu wa Wizara Katiba na Sheria Bi. Mary makondo   akiongea kwenye kikao cha Majadiliano ya   Katiba mpya   na Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba    kilichofanyika kwenye ukumbi Hyatt    Regency   leo tarehe 28 Agosti Jijini Dar es Salaam . Makamu wa kwanza wa Zanzibar wa Rais wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Othamn Masoud Othaman akiwa katika picha ya pamoja na   Mawaziri wakuu wataafu ,   pamoja na meza kuu ( waliosimama )   kwenye kikao Majadiliano ya   Katiba mpya   na Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba    kilichofanyika kwenye ukumbi Hyatt    Regency   leo tarehe 28 Agosti Jijini Dar es Salaam . xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na George Mwakyembe na Lusajo Mwakabuku - WKS- Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi

ZAIDI YA WANANCHI 250,000 WAMEFIKIWA NA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro akiongea na  Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala alipokuwa akiwasilisha wasilisho la Mama Samia Msaada wakisheria Katika shule ya uongozi Kibaha leo tarehe 27 Agosti 2023. Jijini Dar es  Salaam.  Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala  wakimsikiliza Waziri wa Katiba n Sheria Dkt . Damasi Ndumbaro alipokuwa akiwasilisha wasilisho la Mama Samia Msaada wakisheria Katika shule ya uongozi Kibaha leo tarehe 27 Agosti 2023. Jijini Dar es  Salaam.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro amesema katika utekelezaji wa kampeni inayolenga kutoa msaada na elimu ya kisheria kwa wananchi hasa waishio pembezoni, zaidi ya wananchi 250,000 wamefikiwa na huduma hiyo katika mikoa minne ambayo kampeni hii imetekelezwa. Waziri Ndumbaro amesema hayo wakati akitoa wasilisho la vipaumbele vya Wizara ya Katiba na Sheria katika kuhakikisha haki inafikiwa na wananchi wa makundi yote tarehe 26/08/2023 katika mafunzo yaliyoandal

MHE GEKUL AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI MPANGO KAZI WA TAIFA WA HAKI ZA BINADAMU NA BIASHARA

Image
        Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akihutubia katika kikao cha kujadili  Mpango kazi wa Taifa wa Haki za Binadamu na Biashara, kilicho anadaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa Kushirikiana na Shirika na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), katika ukumbi wa  Morena Hotel  tarehe 25 Agosti 2023 jijini Dodoma.         Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Patience K. Ntwina, akizungumza wakati wa kikao cha Kujadili mpango Kazi wa Taifa wa Haki za Binadamu na Biashara kilichoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, leo tarehe 25 Agosti 2023, katika ukumbi wa Hoteli ya Morena jijini Dodoma.   Wawakilishi wa Wizara na Taasisi mbalimbali, wakifuatilia Kikao cha kujadili  Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara, ulioandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa Kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ka

MHE.GEKUL AWASILISHA SHERIA NDOGO KWENYE KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiwasilisha mapendekezo ya Sheria ndogo ya kumlinda mtoa taarifa na ushahidi (WHISTLEBLOWER AND WITNESS PROTECTION ACT, CAP 446) katika kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, katika ukumbi wa Bunge leo tarehe 24 Agosti 2023 jijini Dodoma.   Kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, ikifuatilia wasilisho la sheria ndogo lililowasilishwa kwenye Kamati hiyo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul   katika ukumbi wa Bunge leo tarehe 24 Agost 2023 jijini Dodoma. Mkurugenzi Msaidizi wa Katiba wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Burton A Mwasomola, akichangia katika wasilisho la Sheria ndogo ya Kumlinda Mtoa taarifa na Mshahidi (WHISTLEBLOWER AND WITNESS PROTECTION ACT, CAP 446), katika Kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, katika ukumbi wa Bunge wa  leo tarehe 24 Agosti 2023. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George Mwakyembe, Emmanuel Msenga – WKS       

“TUNABORESHA MIFUMO KWA LENGO LA KUIMARISHA UTENDAJI”- GEKUL

Image
Naibu waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul(MB)akihutubia kwenye hafla ya kuzindu mfumo wa mfumo wa kukusanya, kutunza kumbukumbu za kesi jinai kwenye Ukumbi wa Ofisi za Mashtaka leo tarehe 23 Agosti 2023 Jijini Dodoma. Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe George Simbachawene(MB) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul(MB) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo wakifuatilia uwasilishwaji wa mfumo wa kukusanya, kutunza kumbukumbu za kesi jinai leo tarehe 23Agosti 2023 Jijini Dodoma.  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo akizungumza na Watalaamu kwenye hafla ya kuzinduzi mfumo wa kukusanya, kutunza kumbukumbu za kesi jinai kwenye Ukumbi wa Ofisi za Mashtaka leo tarehe 23Agosti 2023 Jijini Dodoma Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe George Simbachawene(MB) akiwa katika picha ya pamoja na meza kuu  n

KAMATI YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI WA WIZARA NA TAASISI ZAKE

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akitoa ufafanuzi kwenye kikao na ya Kamati ya Kudumu ya bunge Katiba na Sheria wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Wizara kwenye ukumbi wa bunge leo tarehe 22 Agosti 2023.Jijini Dodoma Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara   kwenye kikao kilichofanyika leo tarehe 22 Agosti 2023. Kwenye ukumbi wa bunge Jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akitoa ufafanuzi wa taarifa kwenye kikao cha Kamati ya kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria leo tarehe 22 Agosti 2023. Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na. George Mwakyembe, Emmanuel Msenga, WKS – Dodoma. Kamati ya Kudumu ya Utawala na Katiba na Sheria imepokea taarifa ya utendaji wa Wizara na Taasisi zake na kuipongeza Wizara namna inavyosimamia Taasisi zake katika kutekeleza majukumu yake ikisema kuwa taarifa  inaonesha Wizara  imekuwa na Ushiri

TEHAMA ITAIMARISHA UTAOJI WA MSAADA WA KISHERIA - MAKONDO

Image
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo akiongea na Watalamu wa TEHAMA katika ukumbi wa Morena leo tarehe 22 Agosti 2023 XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amezindua mafunzo ya Mifumo ya TEHAMA yaliyoandaliwa na Shirika la Mtandao wa watoa huduma za Msaada wa Kisheria la (TANLAP) iliyofanyika leo Agosti 22, 2023 Jijini Dodoma. Akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Morena, Katibu Mkuu amesisitiza matumizi ya TEHAMA katika kuwafikia wanyonge na kuwapa huduma za msaada wa Kisheria kote nchini huku akiwaasa washiriki wa mafunzo haya kushiriki kikamilifu Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia yaani Mama Samia Legal Aid Campaign.

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Joseph Mhagama akiongoza kikao cha kamati cha kujadili taarifa ya miezi mitatu ya utekelejazi wa majukumu ya Wizara pamoja na Taasisi zake katika ukumbi wa bunge   tarehe 21 Agosti 2023 jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Katiba  na Sheria  Mhe. Pauline Gekul akiwasilisha taarifa kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika ukumbi wa bunge tarehe 21 Agosti 2023.   Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Sera na Mipngo Bw. Mbaraka Stambuli  akiwasilisha  taarifa ya  utekelezaji wa majukumu ya Wizara  kwenye Kamati ya Kudumu ya bunge Utawala, Katiba na  Sheria  tarehe 21 Agosti 2023. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Joseph Mhagama  akifuatilia taarifa   ya utekelezaji wa majukumu  ya Wizara  ya Katiba na Sheria kwenye kikao kilichofanyika tarehe 21 Agosti 2023 jijini Dodoma.                                                    XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George

RAIS SAMIA ACHANGIA UJENZI WA KANISA LA MT. BARNABA - NGUMBO .

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro  akiongea na waumini wa kanisa la Mt. Barnaba  lilipo Wilaya ya Nyasa  mkoani Ruvuma. tarehe 20 Agosti 2023.  Waumini wa Kanisa la Mt. Barnaba  lilopo  Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma wakifurai baada ya Waziri wa Katiba NaSheria  Mhe. Damas Ndumbaro kuwasilisha mchango wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  tarehe 20 Agosti 2023.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki katika Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Barnaba-Ngumbo lililopo Kijiji cha Ngumbo,Wilaya ya Nyasa.  Katiba Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Mhe. Filberto Sanga, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe.Ndumbaro amewaasa wananchi wa Kijiji cha Ngumbo kuendelea kumcha Mungu na kumjengea Mungu nyumba ya Ibada kwa kuwa Mungu mwenyewe katika maandiko matakatifu ameahidi kutuletea amani kupitia nyumba za Ibada huku akiwaasa viongozi kutekeleza majukumu yao ya kiroho na si kutumika kisiasa kunakopelekea kuwachanganya w

NDUMBARO AHIMIZA USHIRIKIANO BAINA YA TAASISI ZA SERIKALI NA WADAU KATIKA UPATIKAJI HAKI.

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  akiongea na wadau wa haki walihudhuria kongamano hilo jijini Arusha tarehe 17  - 18 Agosti 2023. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akiwahutubia wadau wa haki walihudhuria kongamano hilo jijini Arusha tarehe 17  - 18 Agosti 2023. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  akibadilishana mawazo na Makamu Mwenyekiti wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Bi. Lulu Ng’wanakilala wakiwa katika mapumziko mafupi ya kongamano hilo. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  akiwa katika picha ya pamoja na wadau na menejimenti ya Wizara ya katiba na Sheria. Na. Lusajo Mwakabuku WKS - Arusha  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezitaka taasisi za Serikali hususani zinazoshughulika na masuala ya upatikanaji wa haki, Mahakama pamoja na Bunge kufanya kazi kwa pamoja na wadau wote wa huduma za msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki nchini kwa manufaa ya watanzania wote. Ndu

NDUMBARO AFANYA ZIARA MALINYI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt damasi Ndumbaro   akiwa na wafanakazi wa Malinyi Paralegal unity  alipotembelea ofisini  Malinyi wilaya ya Malinyi  Mkoa wa Morogoro.     Lusajo Mwakabuku: WKS Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Malinyi iliyopo Mkoa wa Morogoro kwa lengo la Kutembelea Wasaidizi wa Kisheria ambapo tarehe 12/08/2023 alitembelea ofisi ya Wasaidizi wa Kisheria Malinyi (Malinyi Para Legal Unity) na kukutana na uongozi Kituo hicho ambacho kimekua na msaada mkubwa katika Wilaya hiyo yenye migogoro ya wakulima na wafugaji.  Katika ziara hiyo, Mhe. Ndumbaro akimbatana na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi bwana Sebastian Waryuba na uongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro wamejadili namna ya kushighulikia masuala mbali mbali ya upatikaji haki Wilayani hapo.  

Dkt. Ndumbaro Aongoza Kikao cha Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.

Image
Bi. Mary Makondo Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria akikaribisha wajumbe kwenye Kikao Kazi cha kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023. Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro akiongoza Kikao Kazi cha kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023. Bw. Abdulrahman Mshamu Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma akitoa wasilisho la mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali kwenye Kikao Kazi kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023.   Bw. Griffin Mwakapeje Katibu Mtendaji wa Tume ya Kubadili Sheria akichangia kwenye Kikao Kazi cha kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023. Na. William Mabusi. WKS Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Da