Posts

Showing posts from March, 2024

KAMATI YAIPONGEZA SERIKALI UJENZI WA JENGO LA WAKILI MKUU WA SERIKALI

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akitoa maelezo ya awali ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Wakili Mkuu wa Serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 27 Machi, 2024 Mji wa Serikali Mtumba Dodoma. Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Mark Mulwambo akitoa maelezo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 27 Machi, 2024 Mji wa Serikali Mtumba Dodoma. Mkandarasi wa mradi Eng. Baraka Mosha akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Wakili Mkuu wa Serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 27 Machi, 2024 Mji wa Serikali Mtumba Dodoma. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo, viongozi kutoka Wizarani na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria mbele ya jengo la Wakili Mkuu wa Serikali linalojengwa  Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, tarehe 27 Machi, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

KAMATI YAPOKEA NA KURIDHIA MAKADIRIO YA BAJETI 2024/25

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 25 Machi, 2024 kwenye Ofisi za Bunge Dodoma. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Florent Kyombo akichangia hoja kwenye kikao cha Kamati hiyo na Wizara ya Katiba na Sheria, tarehe 25 Machi, 2024 kwenye Ofisi za Bunge Dodoma. Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Edward Olelekaita Kisau akichangia hoja kwenye kikao cha Kamati hiyo na Wizara ya Katiba na Sheria tarehe 25 Machi, 2024 kwenye Ofisi za Bunge Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akitoa salaam kwenye Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, baada ya Wizara yake kuwasilisha Makadirio ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 tarehe 25 Machi, 2024 kwenye Ofisi za Bunge Dodoma. Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudum

DKT. CHANA ASISITIZA UADILIFU

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati wa hafla ya kufunga Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, tarehe 22 Machi, 2024 Jijini Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Mbuki Feleshi akihutubia kabla ya kumkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria kufunga Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, tarehe 22 Machi, 2024 Jijini Dodoma. Mawakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria waliokuwa wanashiriki Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, baada ya kupiga kura ya kuwachagua viongozi mbalimbali wa Chama cha Mawakili wa Serikali tarehe 22 Machi, 2024 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewaagiza Mawakili wa Serikali na Maafisa Sheria kuzingatia utawala wa sheria na kuendelea kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuwajenga imani wananchi wanowatumikia. Dkt. Pindi ameyasema hayo alipokuwa anafunga Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Ser

DKT. CHANA AHIMIZA USHIRIKIANO NA UWAJIBIKAJI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati wa kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, tarehe 21 Machi, 2024 Jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza Bi. Mary Makondo akihutubia kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, tarehe 21 Machi, 2024 Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya TUGHE tawi la Wizara baada kuhutubia Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, tarehe 21 Machi, 2024 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewataka watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kuongeza ushirikiano na kila mmoja kutimiza wajibu wake ili kwenda na kasi ya maboresho na mapinduzi makubwa yaliyofanyika ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo kutekeleza mapendekez

JUKUMU LA WANANCHI KUPATA HAKI NI LENU – WAZIRI MKUU

Image
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia wakati akifungua   Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, 21 Machi, 2024 Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) alipotembelea banda la Wizara kabla ya kufungua Mkutano wa Mawakili wa Serikali, tarehe 21 Machi, 2024 Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akipokea Miongozo mbalimbali ikiwemo ya Uandishi wa Sheria na Utoaji wa Huduma ya Msaada wa Kisheria iliyozinduliwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, 21 Machi, 2024 Dodoma. Wakurugenzi wa Wizara ya Katiba na Sheria ambao pia ni Mawakili wa Serikali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, tarehe 21 Machi, 2024 Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amesema

KAMATI YAIDHINISHA BAJETI YA MAHAKAMA KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akijibu hoja kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, tarehe 18 Machi, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma. Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel akisoma Makadirio ya bajeti ya Mahakama kwa mwaka wa fedha 2024/25 mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, tarehe 18 Machi, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma. Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Dkt. Charles Kimei akichangia hoja baada ya Kamati hiyo kupokea Makadirio ya bajeti ya Mahakama kwa mwaka wa fedha 2024/25, tarehe 18 Machi, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma. Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (kulia) akisoma taarifa wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, tarehe 18 Machi, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Daniel Sillo imepokea na kuidhinisha Makadirio ya bajeti ya Mhimili wa Mahakama kw

KAMATI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea wakati akitoa shukrani zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, tarehe 13 Machi, 2024 ilipotembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, wakifuatilia wasilisho la mfumo wa Kunukuu na Kutafsiri mwenendo wa mashauri ya Mahakama, tarehe 13 Machi, 2024, walipotembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwenye picha ya pamoja na Waziri Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel, tarehe 13 Machi, 2024, walipotembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama amesema Kamati imeridhishwa na matumizi ya fedha iliyoidhinishwa Bungeni kutekeleza miradi mbalim

KAMATI YA BUNGE YAKAGUA MRADI WA UJENZI WA IJC NJOMBE

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na Wanahabari wakati wa ukaguzi uliofanywa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwenye Mradi wa ujenzi wa IJC mkoani Njombe. Tareh 13 Machi, 2024. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Kizito Mhagama (wa pili kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) mkoani Njombe tarehe 13 Machi, 2024. Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakichangia wasilisho la taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki kinachojengwa mkoani Njombe na Mahakama ya Tanzania. Tarehe 13 Machi, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WKS, Njombe . Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 13 Machi, 2024 imekagua Mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki IJC kinachojengwa mkoani Njombe chenye thamani ya shilingi t

SUALA LA MIRADI YA SERIKALI KUTOZWA KODI KUFIKISHWA BUNGENI

Image
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza wakati wa ziara ya Kamati yake uwandani mkoani Iringa leo 12/03/2024. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mkoani Iringa, 12/03/2024. Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha taarifaa ya utekelezaji wa Mahakama wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria mkoani Iringa leo 12/03/2024. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Watendaji wa Mahakama na viongozi wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria mkoani Iringa leo 12/03/2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WKS IRINGA Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mh

MAONESHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Image
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametembelea Banda la Wizara ya Katiba na Sheria leo tarehe 9 Machi, 2024 kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma katika kuadhimisha wiki ya Maonesho ya Siku ya Wanawake Duniani.

RAIS MWINYI AFUNGA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI ZA MADOLA

Image
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati anafunga Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, 08 Machi, 2024 Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola MH. Patricia Scotland KC, 08 Machi, 2024 Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kabla ya kufunga Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, 08 Machi, 2024 Zanzibar. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu (kulia) miongoni mwa Viongozi waliohudhuria hafla ya kufunga Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, 08 Machi, 2024 Zanzibar. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola MH. Patricia Scotland KC, kulia kwake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Ma