Posts

Showing posts from September, 2023
Image
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan. 27/09/2023 Jijini Dar es Salaam. Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan (kulia) alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana. 27/09/2023 Jijini Dar es Salaam. Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea alipokutana na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan. 27/09/2023 Jijini Dar es Salaam. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan na kufanya majadiliano ya namna bora ya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali hasa katika Sekta ya Sheria. Kikao hicho kimefanyikia tarehe 27/09/2023 katika Ukumbi wa Ofisi za Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) Jijini Dar es Salaam ambapo moja ya eneo lililogusiwa katika mazungumzo hayo ni kuimarisha mifumo ya Haki ambapo Balozi Avetisyan ameahidi

“UKIKIUKA UTII WA SHERIA UTAENDELEA KUWA MTEJA WETU” WAZIRI CHANA.

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Iringa leo tarehe 25 Septemba 2023.   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akiongea na watumishi wa ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Iringa leo tarehe 25 Septemba 2023. Watumishi wa ofisi Taifa ya Mashtaka mkoa wa Iringa wakimsikiza waziri wa katiba na sheria Mhe. Balozi Pindi Chana alipofanya ziara katika ofisi hizo mkoani Iringa leo tarehe 25 Septemba 2023. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika  picha ya pamoja watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa Iringa leo tarehe 25 Septemba 2023.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX  Na, George Mwakyembe – WKS Iringa.  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana amekemea vikali vitendo vyote vya ukatili unaofanywa na baadhi ya watu katika jamii zetu na kuwakumbusha kuwa vyombo vya haki anavyovisimamia vipo imara na makini katika kuhakikisha kila mtanzania anaishi

MSLAC YAREJESHA VIWANJA VIWILI ALIVYOPORWA MWANANCHI

Image
  Bi. Mboje Masanja Ndahile Mkazi wa eneo la Imalilo Kata ya Bunamhla ,  Halmashauri ya Mji wa Bariadi akifurai baada ya kurudishiwa shamba lake  kupitia Mama Samia Legal  Aid Campain mkoani Simiyu.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Bariadi Mgogoro uliodumu kwa miaka miwili kati ya Bi. Mboje Masanja Ndahile Mkazi wa eneo la Imalilo Kata ya Bunamhla na Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambao haukumpa matumaini ya kupata viwanja vyake viwili umetatuliwa na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign - MSLAC) kwa siku tatu na mama huyo kurejeshewa viwanja vyake. Jitihada za kupata viwanja hivyo zilikuwa zimegonga mwamba kwani kila alipokuwa anafuatilia aliambiwa Serikali imechukua viwanja hivyo ili kupanga mji na hakukuwa na namna nyingine ya kuvipata. “niliposikia kuna kongamano la sheria na watu wanasaidiwa nilikuja na kuonana na wataalam wa sheria akiwepo kiongozi wenu na akaagiza nipate viwanja vyangu na kweli nimevipata hizi hapa

WAZIRI CHANA AIPONGEZA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria leo tarehe 22 Septemba 2023 Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria katika ofisi zao zilizopo udom leo tarehe 22 Septemba 2023 Jijini Dodoma.    Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Balozi Dkt. Pindi Chana katika ofisi zao zilizopo UDOM leo tarehe 22 Septemba 2023 Jijini Dodoma.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe & Faraja Mhise - WKS. Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na menejimenti pamoja watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria ikiwa ni muendelezo wa ziara zake zenye lengo la kuyafahamu majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Wizara hii.   Akiongea na watumishi hao leo tarehe 22 Septemba, 2023 katika ofisi za Tume ya Kurekebisha She

DKT PINDI CHANA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA

Image
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana, Waziri wa Katiba na Sheria na baadhi ya Viongozi wa Wizara kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia baada ya kufanya nao mazungumzo juu ya ushirikiano katika kuendeleza sekta ya sheria nchini, tarehe 20/09/2023 kwenye ofisi za RITA Jijini Dar es Salaam. Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana, Waziri wa Katiba na Sheria alipokutana na ujumbe wa Benki ya Dunia tarehe 20/09/2023 Jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za RITA na kuzungumza juu ya ushirikiano katika kuendeleza sekta ya sheria nchini.

WAZIRI CHANA AKEMEA MIMBA ZA UTOTONI

Image
Meza Kuu ikiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria bada ya uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign mkoani Simiyu tarehe 18 Septemba, 2023 Mjini Bariadi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati anazindua utekelezwaji wa Mama Samia Legal Aid Campaign mkoani Simiyu tarehe 18 Septemba, 2023 Mjini Bariadi. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi & Lusajo Mwakabuku – WKS Simiyu  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (MB) amekemea mimba za utotoni akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanahudhuria shuleni kwa faida yao ya baadaye na kujenga taifa imara, lenye kizazi bora na wataalam wengi zaidi. Mhe. Waziri Chana ameyasema hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Bariadi waliohudhuria uzinduzi wa utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Mama Samia Legal Aid Campaign tarehe 18 Septemba, 2023. Kampeni hiyo itafanyika mkoani humo kwa siku kumi kwa kutoa elimu ya sheria na utatuzi wa

WAZIRI KATIBA NA SHERIA AIPONGEZA MAHAKAMA KWA KUIHESHIMISHA TANZANIA KIMATAIFA

Image
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na Viongozi wengine kwenye picha ya pamoja na wageni wake – Waziri wa Katiba na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria walipomtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, 15/09/2023.                                         XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na. Faustine Kapama-Mahakama na Sade Soka-UDSM Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Pindi Chana tarehe 15 Septemba, 2023 amemtembelea Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo mafupi ambapo ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kuiheshimisha Tanzania kimataifa. Mhe. Balozi Chana, ambaye aliongozana na Naibu Waziri, Mhe. Pauline Gekul na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma kutoka Wizara hiyo, Bw. Abdulrahman Mshamu, amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambayo masuala ya utawala wa Sheria yanazingatiwa. “Tunapata fursa wakati mwingine kwenda Nchi mbalimbali, ukienda huko duniani ndipo ut

VIJANA JITUMENI KATIKA MASOMO FURSA KWENYE KADA YA SHERIA NI NYINGI - CHANA

Image
  Waziri wa katiba na sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (MB) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi, Viongozi na Wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania pamoja na Viongozi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (MB) akiongea na Wanafunzi wanaoendelea na masomo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) alipokuwa akifanya ziara yake ya kwanza tangu kuapishwa kwake kuwa Waziri wa Katiba na Sheria leo tarehe 12/09/2023.   Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof. Sist J. Mramba akimtembeza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (MB) katika viunga mbalimbali vya Taasisi hiyo alipofika mahali hapo ikiwe ni sehemu ya Ziara yake jijini Dar es salaam. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku – WKS Dar es salaam Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (MB) amewataka Wanafunzi wanaoendelea na masomo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Kwa Vi

GEKUL ASHIRIKI “UTU KWANZA RUN” DAR ES SALAAM

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akizindua mradi wa Dawati la Msaada wa Kisheria (Legal Aid Desk Project), tarehe 10 Septemba, 2023 Jijini Dar es Salaa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akishiriki mbio kwenye hafla ya Utu Kwanza Run ambapo alikimbia kilomita tano, tarehe 10 Septemba, 2023 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiwasilisha hotuba yake kwenye hafla ya Utu kwanza Run kwenye Viwanja vya Leaders Club tarehe 10 septemba 2023 Jijini Dar es slaam .  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na. Lusajo Mwakabuku – WKS Dar es salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, ameungana na Wakimbiaji, Watembeaji na Waendesha Baiskeli walioshiriki “Utu Kwanza Run” tarehe 10 Septemba, 2023 Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zilizoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) la Utu Kwanza, chini ya Uenyekiti wa Wakili Shehzada Amir Walli zimele

DKT. CHANA AITAKA TUME KUWA NA MKAKATI WA KUZUIA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU

Image
Waziri wa Katiba n Sheria  Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana  akihutubia  kwenye kikao na Wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,  Tarehe 07 Septemba 2023 Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi, Emmanuel Msenga na Faraja Mhise – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini kuwa na mkakati wa kuzuia mambo yanayosababisha uvunjifu wa haki za binadamu ili hali ya amani iendelee kutawala nchini. Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo alipotembelea ofisi za Tume hiyo maeneo ya Kilimani na kuhutubia wafanyakazi wa ofisi hiyo tarehe 07 Septemba, 2023 Jijini Dodoma. “ Pamoja na kuandika na kutoa taarifa za uvunjifu wa haki za binadamu  nchini   lakini pia tuwe na mkakati wa kuzuia mambo hayo yasitokee na eneo sahihi la kutekeleza hili ni  T ume yetu inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu na utawala bora. ” Alisema Dkt. Chana. Balozi Dkt. Chana ameiponge