Posts

Showing posts from November, 2020

MKUU WA MKOA WA TANGA ATAKA TAASISI ZA UTOAJI HAKI ZIBORESHWE ILI ZIWEZE KUTOA HAKI KWA WAKATI

  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigella ataka taasisi za utoaji haki ziendelee kuboreshwa ili haki iweze kupatikana kwa wakati. Mhe. Shigella aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa kamati za usalama za mkoa na Wilaya, kamati za maadili ya Mahakimu na Kamati za Parole mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria. Mhe. Mkuu wa Mkoa aliwaambia viongozi hao kuwa wana dhamana kubwa ya kuhakikisha nchi ina utulivu, amani na usalama hivyo waitumie fursa hii ya kupata mafunzo hayo vizuri na kushirikishana na wengine. “Tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha utulivu, usalama na amani ya nchi tunaitimiza kwa Pamoja, tutumie fursa hii vizuri na tushirikishane” alisema Mhe. Shigella. Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema mamlaka za kutenda haki mkoani humo ikiwemo Mabaraza ya ardhi ya kata yamekuwa yakilalamikiwa sana kutokana na ufanisi wake ambao unasababishwa na watumishi wachache waliopo ambayo inasababisha ucheleweshwaji wa majukum

WAJUMBE WA MABARAZA YA ARDHI ACHENI KUPOKEA RUSHWA – MHE. NGUVIRA

  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Mhe. Toba Nguvira awaasa wajumbe wa mabaraza ya ardhi wilayani humo kuacha tabia ya kupokea rushwa na kunyima haki wananchi. Mhe. Nguvira aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya utawala bora, Wosia na Mirathi kwa watendaji kata na wenyeviti wa mabaraza ya ardhi wilayani humu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria ambayo kitaifa yalizinduliwa tarehe 12 Mkoani Tanga. Mkuu wa wilaya huyo aliwaambia watendaji kata na wenyeviti wa mabaraza ya kata hao wayatumie mafunzo hayo vizuri ili kumaliza migogoro mingi iliyopo ambayo inaanzia kwenye kata na inasababishwa na rushwa na hivyo kunyima haki baadhi ya wananchi. “Migogoro ya ardhi na mirathi ni mingi sana nchini na inasababishwa na rushwa” alisema Mkuu wa wilaya huyo. Aidha Mhe. Nguvira alisema sheria zimewekwa kuhakikisha haki inatendeke kwani kukosekana kwa haki kunapelekea machafuko katika jamii. Mhe. Nguvira aliwasisitiza wajumbe w

WATANZANIA TUWE NA UTAMADUNI WA KUANDIKA WOSIA KUEPUKA CHANGAMOTO ZA MIRATHI- JAJI MRUMA

  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Tanga Mhe. Jaji Amir Mruma amesema watanzania tuwe na utamaduni wa kuandika wosia kwani suala la usimamizi wa mirathi huwa linakuwa rahisi sana pale kunapokuwa na wosia wa marehemu kuhusu mgawanyo wa mali zake pindi atakapoondoka duniani. “Mara nyingi wosia umekuwa ukirahisisha na kuondoa migogoro ya umiliki wa mali za marehemu na pia umekuwa ukibainisha nani atasimamia mali hizo kwa maendeleo ya familia husika” alisema Jaji Mruma. Jaji Mruma ameyasema hayo wakati akizindua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria yanayofanyika kitaifa Mkoani Tanga kuanzia tarehe 12 hadi 18 Novemba, 2020 yakilenga kupunguza changamoto za kisheria kwa wananchi. Mhe. Jaji Mruma alisema kwa utafiti walioufanya baada ya kukaa muda mrefu mahakamani wamegundua changamoto kubwa zaidi ya mirathi katika jamii inasababishwa na familia nyingi kutoandika wosia mapema kabla ya kufariki. Aliongeza kuwa usimamaizi