Posts

Showing posts from June, 2023

MKUTANO WA 77 WA HAKI ZA BINADAMU NA WATU KUFANYIKA JIJINI ARUSHA

Image
 Naibu Waziri wa  Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) akiongoza kikao kazi cha maandalizi ya Mkutano wa 77 wa Haki za Binadamu . tarehe 28 Juni 2023 Jijini Arusha                                                        XXXXXXXXXXXXXXXXXXX William Mabusi - WKS Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) ameongoza timu ya Wizara kwenye Kikao Kazi kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa 77 wa Haki za Binadamu na Watu utakaofanyika hapa nchini mnamo tarehe 20 Oktoba mpaka 9 Novemba, 2023 mkoani Arusha na kuagiza usimamizi mzuri wa maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo. Kikao Kazi hicho kimefanyika Jijini Arusha tarehe 28 Juni, 2023 na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Makondo, Mwenyeji Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. John Mongella, ndugu Steven Zelothe  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha miongoni mwa wengine. Akiongea katika Kikao Kazi hicho Bi. Makondo alielezea chimbuko la Mkutano huo na alisema ni heshima kwa nchi kuwa mwenyeji wa Mkutano huo akiba

Wizara ya Katiba na Sheria yakutana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola

Image
  Wawakilishi kutoka RITA wakifafanua jambo kuhusu namna taasisi ya RITA inavyofanya kazi wakati wa kikao na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola. Tarehe 28 Juni 2023 Jijini Dodoma  Mwenyekiti wa Sekretarieti ya tathimini kutoka Jumuiya ya Madola Bi. Evelyn Pedersen (wa nne kulia) akitoa ufafanuzi mbele ya watalaamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake, Tarehe 28 Juni 2023 Jijini Dodoma. Bi. Evelyn Pedersen (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma Ndg. Abdulrahman Mshamu pamoja na watalaam wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake, Tarehe 28 Juni 2023 Jijini Dodoma. George Mwakyembe- WKS Wizara ya Katiba na Sheria wamefanya kikao na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola. Katika kikao hicho ambacho kimeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma Ndg. Abdulrahman Mshamu akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizra ya Katiba na Sheria.    Ka

Tufanye kazi na kushiriki kwenye Michezo: Dkt. Ndumbaro

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akipokea medal ambazo Wizara ilishinda kwenye Marathon ya miaka 60 ya JKT, tarehe 27 Juni, 2023. Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa kwenye hafla ya kuwapongeza watumishi walioshiriki kwenye marathon ya miaka 60 ya JKT, tarehe 27 Juni, 2023.                                            XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi - WKS Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesisitiza watumishi wa Wizara hiyo pamoja na kutekeleza majukumu yao lakini pia washiriki kwenye michezo kwani michezo huimarisha afya. Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo tarehe 27 Juni, 2023 wakati wa hafla ya kuwapongeza watumishi walioshiriki kwenye marathon ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kufikisha miaka 60 iliyofanyika tarehe 25 Juni, 2023 ambapo Wizara ilishiriki na kuwa miongoni mwa Wizara zilizopata Medali, Mgeni Rasmi kwenye marathon hiyo alikuwa Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Aidha, Waziri alisisitiza watumishi

WAHARIRI WAPEWA MAFUNZO YA SHERIA NA KANUNI ZA ULINZI KWA WATOA TAARIFA NA MASHAHIDI

Image
 Mkurugenzi wa Idara ya Katiba n Sheria  Ndg. Khalist Luanda ambaye ndiye  mwezeshaji wa  mafunzo haya akitoa wasilisho kwa wahariri na wanahabari wandamizi walioshiriki mafunzo hayo 24.Juni 2023. Singida   Jesse Kwayu  Mhariri mwandamizi akiuliza swali katika kikao cha  mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria  Jukwaa la wahariri singinda leo tarehe 24Juni 2023. Sehemu ya Wahariri  na waandishi  waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari na watumishi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria  wakiendelea na mafunzo mjini Singida .                                                         XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku – WKS Singida Wizara ya Katiba na Sheria imefanya mafunzo kwa Wahariri na Wanahabari Waandamizi wa Vyombo mbalimbali vya Habari juu ya Sheria ya kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Ulinzi wa Mashahidi, Sura ya 446 (The Whistleblower and Witness Protection Act, Cap 446) kwa lengo la kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini.

ONGEZENI JUHUDI KATIKA UTOAJI ELIMU YA SHERIA KWA UMMA: GEKUL

Image
 Naibu Waziri  wa Katiba na Sheria  Pauline Gekul akiongea na watumishi wa Tume ya Kurekebisha sheria hawapo picha  tarehe 22 Juni 2023 jijini Dododma .                                                   XXXXXXXXXXXXXXXXX  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amewataka watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria   kuongeza juhudi katika suala la utoaji elimu kwa umma kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisheria ili jamii iweze kuzitambua Sheria zilizopo nchini na kuwasaidia kuzitumia hususan pale ambapo wanapotaka kufahamu haki zao juu ya  jambo husika. "Kiu kubwa ya jamii ipo kwenye elimu, sheria tunazo nyingi sana zimetungwa lakini jamii zetu haizifahamu sheria hizo na wengi wanateseka kupata haki zao kupitia sheria kwasababu hawana elimu ya kutosha ya kuzijua sheria hizo."  Mhe. Gekul amebainisha hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Tume hiyo iliyofanyika tarehe 22 Juni, 2023 Jijini D

MKUU WA WILAYA AWANYOOSHEA KIDOLE WATUMISHI WA ARDHI

Image
 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga  Bi. Johari Musa Samizi  akipokea mrejesho  wa utekekelezaji wa Mama Samia Legal Aid Campain iliyokuwa inafanyika kwenye  yake . tarehe 21 Juni 2023.                                               XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Shinyanga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johari Musa Samizi amewataka watumishi wa ardhi kufanya kazi kwa kufuata haki na taratibu za kazi wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku katika kuwahudumua wananchi ili kuepuka kusababisha migogoro ya ardhi nchini. Bi. Samizi ameyasema hayo wakati timu zilizokuwa zinatekeleza kampeni ya kitaifa ya Mama Samia Legal Aid Campaign kwenye Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga zilipofika ofisini kwake tarehe 21 Juni, 2023 kutoa mrejesho wa utekelezaji wa kampeni hiyo iliyokuwa inatekelezwa mkoani humo kwa siku kumi kuanzia tarehe 11 hadi 20 Juni 2023. Mtumishi anafanya anachojua na siyo kwamba hajui anachofanya, anajua kabisa hapa nachakachua na ha

Wizara imejipanga kuendelea kujenga Mahakama nchini - Pauline Gekul.

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Pauline Gekul aitoa ufafanuzi wa swali aliloulizwa   na mbunge wa kigoma kusini mheshimiwa Nashon Bindyanguze leo tarehe 20 juni 2023   Bungeni Dododma.                                                    XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na. George Mwakyembe. WKS – Dodoma. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amesema Wizara imejipanga kundelea na ujenzi wa Mahakama nchini kwa mwaka wa bajeti 2023/2024 na tayari Wizara imejipanga kujenga zaidi ya mahakama 60. Mheshimiwa Gekul amesayema hayo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kigoma mheshimiwa Nashoni Bindyanguze mbunge wa Kigoma Kusini. Mheshimiwa Gekul amesema kwa mwaka wa bajeti 2024/2025 Wizara itajenga Mahakama ya Mwanzo katika eneo la Mgambo ambalo ndiyo makao makuu ya Tarafa ya Buhingu. Naye mbunge wa Arusha mjini Mhe. Mrisho Gambo aliuliza swali la nyongeza kwa mheshimiwa Naibu Waziri Gekul kutaka Kujua ujenzi wa mahakama ya mwanzo katika kata ya Terati. Mheshimiwa Ge

TULISTAHILI ELIMU HII: WAKAZI WA SALAWE

Image
 Wakili  wa Kujitegemea Ndg. Chrisatus Chegula akitoa elimu ya sheria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Salawe Halmashauri ya Shinyanga  tarehe 16 Juni, 2023                                                     XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Shinyanga   Wananchi wa Kata ya Salawe na Solwa wamesema walistahili kupata elimu ya sheria na kupatiwa huduma ya msaada wa kisheria kutokana na kuishi bila kujua sheria inasemaje kwenye maeneo mengi na kutokujua wapi wapeleke mashauri yao hasa ya ardhi baada ya kutofautiana na maamuzi ya mamlaka za chini na kutokujua namna ya kushughulikia kero za wasimamizi wa mirathi.   Mikutano katika Kata hizo mbili imefanyika kwa nyakati tofauti tarehe 16 Juni, 2023 ikiwa ni utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Sheria (MSLAC) katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga. Bwana Heleman Mathias Sanane wa kijiji cha Mwanga Songambele kutoka Kata ya Salawe ameishukuru elimu ya sheria inayotolewa kwenye Kampeni hiyo kwa kusema "wanan

MADAWATI YA JINSIA SI KWA AJILI YA WANAWAKE PEKEE - MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA

Image
 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga  Bi. Johary Shamizi ( wa tatu kulia ) katikati  kwenye picha ya pamoja na timu ya Mama Samia Legal Aid Campain (MSLAC) walipofika  ofisini  kwake kujitambulisha  tarehe 12 juni 2023.                                                     XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Shinyanga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johary Shamizi amesema moja ya sababu za wanaume kushindwa kujitokeza kutoa malalamiko yao kwenye dawati la jinsia ni kwa kuwa hawapendi malalamiko yao kusikilizwa na mwanamke hali inayofanya kujikuta wanakosa msaada hata pale wanapouhitaji. Bi. Shamizi ameyasema hayo tarehe 12 Juni, 2023 alipokutana na kuzungumza na timu ya wataalam wa MSLAC waliofika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo mengine alipongeza jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuona wananchi wengi wa hali ya chini wanapata elimu ya sheria na kuwaagiza wananchi hususan wanaume kujitokeza kwa wingi katika kampeni hiyo kupata elimu juu ya ukatili

SHINYANGA BADO YAANDAMWA NA UKATILI WA KIJINSIA

Image
 Afisa Ustawi wa Jamii wa Hospital ya Mkoa wa Shinyanga  ambaye ni mmoja  wa watalaam wanaotekeleza  Mama Samia Legal Aid Campain( MSLAC ) Mkoani Shinyanga bwana Leopold Hamza akizungumza na wananchi .                                                            xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WKS Shinyanga Mkoa wa Shinyanga umetajwa kuendelea kukabiliwa na matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo, mimba na mauaji na sababu kuu ikitajwa kuwa ni jamii kuendelea kushikilia mila na desturi zilizopitwa na wakati, elimu ndogo pamoja na jamii kutokuwa tayari kutoa taarifa ya matukio hayo. Afisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambaye ni mmoja wa wataalam wanaoetekeleza Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) mkoani humo, bwana Leopold Hamza aliyasema hayo wakati akitoa elimu ya kijinsia wakati timu hiyo ya wataalam ilipokutana na wananchi wa vijiji vya Mwamagunguli na Galamba vya kata ya Kolandoto mkoani Shinyanga ambapo mada mbalimbali za kisheria pa