Posts

Showing posts from September, 2022

RAIS SAMIA ATAKA SHERIA YA KULINDA UWEKEZAJI IANGALIWE UPYA

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akizindua Chama cha Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba, 2022 jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba, 2022 jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Mfumo wa Usajili wa Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba, 2022 jijini Dodoma. Sehemu ya Mawakili wa Serikali wakimsikiliza Rais. XXXXXXXXXXXXXXXXXX Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia upya sheria ya Uwekezaji nchini ili kuepuka migongano na migogoro kati ya nchi na Wawekezaji.   Rais Samia ameyasema hayo wakati akizindua Chama cha Mawakili wa Serikali katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre leo tarehe 29 Septemba, 2022, ambapo yeye a

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE GEOPHREY MIZENGO PINDA(MB) AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA SHIRIKA LA MASHAURIANO YA SHERIA ZA KIMATAIFA JIJINI NEW DELHI NCHINI INDIA

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXX Leo tarehe 26.09.2022 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Mizengo Pinda ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 60 wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria za Kimataifa la Nchi za Asia  na Afrika (AALCO) uliofanyika Jijini New Delhi nchini India. Katika Mkutano huu Mhe. Naibu Waziri amewasilisha salamu za shukrani kama Rais wa 59 wa Shirikisho hilo  anayemaliza muda wake. Mkutano huu unaofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Septemba 2022, masuala mbalimbali yanatarajiwa kujadiliwa ikiwemo Mabadiliko ya Tabia Nchi, Biashara na uwekezaji, Mazingira na Ugaidi, Masuala ya Wakimbizi na Tume ya kimataifa inayoshughulikia maendeleo ya Sheria za Kimataifa  Katika Mkutano huu Mhe. Naibu Waziri ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini India, Bi Hanisa Mbega, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt  Khatibu Kazungu, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria Wizara ya Katiba na Sheria Bwana Griffin Mwakapeje na Ofisa wa Wizara wa Mambo ya Nje Kitengo cha Sheria Bwa

SERIKALI YADHAMIRIA KUWEKA MISINGI THABITI KATIKA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA HAKI – KATIBU MKUU MAKONDO

Image
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akifungua kikao cha Wakuu wa Taasisi cha kupokea maoni kuhusu Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mashtaka ya Mwaka 2022. Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Emmanuel Mayeji akimkaribisha Katibu Mkuu kufungua kikao. Washiriki wakichangia mada. Washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXXXXXXX Serikali ya Tanzania imedhamiria kuweka misingi thabiti ya kisera na kiutawala katika kuimarisha upatikanaji wa haki jinai nchini. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo wakati akifungua kikao cha Wakuu wa Taasisi cha kupokea maoni kuhusu rasimu ya Sera ya Taifa ya Mashtaka ya mwaka 2022 leo tarehe 26, Septemba 2022 Mkoani Singida. Bi Makondo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya maboresho katika mifumo ya Haki Jinai, maboresho hayo yanalenga kuimarisha mifumo ya kiutawala na kiutendaji katika kuendesha mashauri ya jinai nchini. ‘’Matokeo ya mabores

WABUNGE WAPATIWA SEMINA KUHUSU MAREKEBISHO YA SHERIA YA NDOA

Image
                                                 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akichangia mada.                                                  Naibu Waziri Mhe. Geophrey Pinda akichangia mada.   Wabunge wakisikiliza mada  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yapatiwa semina kuhusu marekebisho ya sheria ya ndoa ya Mwaka 1971. Semina hiyo kwa Wabunge imetolewa na Wataalam wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 21 Septemba, 2022. Katika semina hiyo Serikali imesema imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni kutoka makundi mbalimbali ya wananchi Ili kuona namna bora ya kufanyia marekebisho sheria hiyo. Katika mjadala wa semina hiyo jambo kubwa lililojitokeza ni umri sahihi wa mtu kuoa au kuolewa na namna umri  unavyotafsiriwa katika suala hilo Kwa upande wa dini. Dkt. Ndumbaro amesema katika sheria ya ndoa sio kila kitu hakifai, vipo ambavyo vitaendelea kuwepo. Aidha, W

BUNGE LIMERIDHIA ITIFAKI YA KUIONGEZEA MAMLAKA MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha hoja ya kuliomba Bunge kuridhia itifaki ya kuiongezea mamlaka Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. XXXXXXXXXXXX Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia itifaki ya kuiongezea mamlaka  Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hoja ya kuomba kuridhiwa kwa Itifaki hiyo limewasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo, Septemba 20, 2022 kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika wasilisho hilo Dkt. Ndumbaro amesema kuridhiwa kwa Itifaki hiyo kutawezesha nchi wanachama kuwa na Umoja wa Forodha, Soko Huria, Sarafu ya Pamoja na kuwezesha wananchi kuwa na haki ya kuishi kwenye nchi yoyote kati ya nchi wananchama bila bughudha ili mradi uwe na shughuli halali. Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akichangia hoja wakati wa wasilisho hilo amesema itifaki hii itatufaa sana nchi na wananchi wa Tanzania kwani itawezesha wananchi hususan wafanyabiashara kuingia

SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA WAJIBU WA KULINDA HAKI ZA BINADAMU NA WATU – WAZIRI NDUMBARO

Image
                                             Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza                                              kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa                                                 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.                                                       Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary                                                                                                   Makondo   akizungumza  kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20                                                 tangu kuanzishwa kwa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.                                                        Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akipokea Tuzo                                              kwa niaba ya Rais  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.                                                   Samia Suluhu Hassan. XXXXXXXXXXXX

DKT. KAZUNGU AWATAKA WADAU WA MAZINGIRA WASHIRIKI KATIKA UPANDAJI NA UTUNZAJI WA MITI KATIKA MAZINGIRA WALIYOPO

Image
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akipanda mti katika zoezi la upandaji miti katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akiongoza maandamano katika zoezi la upandaji miti katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akizungumza katika zoezi la upandaji miti katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. XXXXXXXXXXXXXX Naibu Katibu Mkuu wa   Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu amewataka wadau wote wa Mazingira kushiriki katika upandaji na utunzaji wa miti katika mazingira waliyopo ili kutekeleza Mkakati wa Utekelezwaji wa Sera ya Taifa ya Uhifadhi wa Mazingira wa mwaka 2020/21. Dkt. Kazungu ameyasema hayo wakati wa tukio la upandaji miti ikiwa ni mojawapo ya shughu

WAZIRI NDUMBARO AZINDUA KAMPENI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA

Image
  XXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amezindua  kampeni ya utoaji wa huduma za  msaada wa Kisheria tarehe 8 Septemba 2022, Jijini Arusha.    Wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Ikiding'a, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Dkt. Ndumbaro amesema Utoaji wa hudumu za msaada wa kisheria utamsaidia mwananchi mnyonge kupata huduma za Mawakili pasipo na malipo.    "Serikali inatambua kuwa siyo kila mwanachi ana uwezo wa kulipia gharama za kisheria, hivyo katika huduma hii tuna wadau mbali mbali ambao tunashirikiana nao  kama vile TLS, TAWLA, Asasi za kiraia, pamoja na wadau wengine". alisema Dkt. Ndumbaro   Aidha, Dkt. Ndumbaro ameshiriki pia kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa  kuhudumia wananchi mbali mbali kama Wakili.   Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda, Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu.  

NAIBU WAZIRI PINDA AWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na Menejimenti ya RITA.   Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akizungumza na Menejimenti ya RITA. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatib kazungu akizungumza na Menejimenti ya RITA. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXX Naibu waziri Mhe. Geophrey Mizengo Pinda amewataka watumishi kuheshimu na kuzingatia Sheria za utumishi wa Umma sambamba na kuheshimiana kila mmoja wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku.   # Ameyasema hayo leo tarehe 6 Septemba, 2022 Jijini Arusha wakati akizungumza na Menejimenti ya RITA katika kikao kazi Cha kuwajengea uelewa katika kuzingatia kanuni, miongozo ya utumishi wa Umma ili Kuunga mkono jitihada za Serikali za kiwaletea Maendeleo wananchi.    #Mhe. Pinda ameongeza kuwa Menejimenti inatakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi na kufuata misingi ya Sheria, uadilifu na busara hasa itakapotokea mtumishi amekwenda kinyume na kutakiwa kuchukuliwa