Posts

Showing posts from July, 2023

Tusiwe Chanzo cha Migogoro Tutatue Kero za Wananchi – Gekul

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akiongea na wananchi wa Kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipotembelea na kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akisikiliza malalamiko ya Ndg. Victory Luena mkazi wa Kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipotembelea na kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akionge na wananchi wa kijiji cha Liuli kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipokuwa akirejea kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023 XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe - WKS Nyasa .   Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) amefanya ziara na kukutana na wananchi wa Kata ya Liuli Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma tarehe 30 Julai, 2023. Akiwa katika ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria

Elimu ya sheria itumike kupunguza ukatili kwenye ndoa: Gekul

Image
Afisa Tarafa ya Matemanga Wilayani Tunduru Bw. Emilian Njogopa akimkaribisha Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Pauline Gekul kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika tarafani humo, tarehe 28 Julai, 2023. Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Pauline Gekul akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika tarafa ya Matemanga Wilayani Tunduru, tarehe 28 Julai, 2023. Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Pauline Gekul akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika tarafa ya Matemanga Wilayani Tunduru, tarehe 28 Julai, 2023. XXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Tunduru   Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) ametoa wito kwa jamii kutumia elimu ya sheria inayotolewa kwenye Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Sheria ya Mama Samia kupunguza na hatimaye kumaliza ugomvi kwenye familia zao na hivyo kuwa na jamii yenye amani ili kukuza maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Mhe. Gekul ametoa wito huo wakati akihutubia wananchi wa vijiji v

Wananchi waomba vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri zaidi ya miaka mitano vitolewe kwenye Ofisi za Kata

Image
Bw. Mwinyijuma Maneno Moshi Afisa Msajili Msaidizi RITA na mtaalam kwenye timu ya kutoa msaada wa sheria ya Mama Samia akitoa elimu ya Usajili wa Vizazi na Vifo kwenye mkutano uliofanyika ofisi za Kata ya Chiwana wilaya ya Tunduru, 26/07/2023.   Wakili Gloria Baltazari kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika na mtaalam kwenye timu ya kutoa msaada wa sheria ya Mama Samia akitoa elimu ya sheria kwenye mkutano uliofanyika ofisi za Kata ya Chiwana wilaya ya Tunduru, 26/07/2023. Bw. Nelson William Afisa Ustawi wa Jamii na mtaalam kwenye timu ya kutoa msaada wa sheria ya Mama Samia akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwenye mkutano uliofanyika ofisi za Kata ya Chiwana wilaya ya Tunduru, 26/07/2023                                            xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Tunduru   Wananchi wa vijiji vya Chiwana, Umoja na Mkandu wilayani Tunduru wameiomba Serikali kuweka utaratibu ili vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri zaidi ya miaka mitano navyo vitolewe kwenye

Elimu tuliyoipata itaondoa migogoro ya mirathi

Image
  Wanakijiji cha Kijiji cha Ngingama kata ya Linga wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji Haki Bi. Beatrice Mpembo baad a ya kikao, tarehe 26 Julai 2023.   Wananchi wa Kijiji cha Ngingama wakisikiliza maada iliyokuwa ikiwasilishwa na Bi. Beatrice Mpembo, tarehe 26 Juali 2023.                                         Bi Beatrice Mpembo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya ufuatiliaji Haki akiwasilisha maada kuhusu ukatili wa kijinsia  tarehe 26 Julai 2023.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe- WKS Nyasa Wanakijiji wa kijiji cha Ngingama Kata ya Linga Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wameshukuru Serikali kupitia Kampeni ya Mama Samia msaada wa kisheria kwa kuwapatia elimu juu ya mirathi ambayo imekuwa ikichangia kuleta migogoro ya ardhi katika jamii yao. Akiongea kwenye mkutano uliofanyika tarehe 26 Julai, 2023 katika ofisi za kata ambapo watalaam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na taasisi zingine za kisheria zilitoa mada mbalimba

MABARAZA YA USULUHISHI YA KATA YAPEWE MAFUNZO YA MARA KWA MARA

Image
  Bw. Walter Kaijage Mwanasheria wa Wilaya ya Tunduru akitoa elimu ya ardhi kwenye mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Masugulu Kata ya Marumba Wilaya ya Tunduru, 25/07/2023. Bw. Mwinyijuma Maneno Moshi Afisa Msajili Msaidizi RITA akitoa elimu ya Mirathi na Wosia kwenye mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Marumba Kata ya Marumba Wilaya ya Tunduru, 25/07/2023. Bi. Mujo Mtani Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto wilaya ya Tunduru akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwenye mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Masugulu Kata ya Marumba Wilaya ya Tunduru, 25/07/2023. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Tunduru Wanakijiji cha Masugulu Kata ya Marumba wameomba Serikali kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara Wajumbe wa Mabaraza ya Usuluhishi ya Kata kuwawezesha kufanya jukumu la usuluhishi kwa ufanisi na hivyo kusaidia kumaliza migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi kwenye ngazi za Kata. Ushauri huo umetolewa kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika tarehe 25 Julai, 2023 kwenye vijij

TUPINGE NDOA ZA UTOTONI NI ADUI WA NDOTO ZA MABINTI WETU.

Image
Mkurugenzi msaidizi wa Haki za Binadamu Ndg. Richard Kilanga akiongea na Wananchi wa kijiji cha Mtipwili kuhusu ukatili wa kijinsia, miradhi, migogoro ya ardhi pamoja na ndoa za utotoni wakati wa utekelezaji wa Mama Samia Leagal Aid Campain Wilaya Nyasa Mkoa wa Ruvuma. Msaidizi wa kisheria ndugu Nurdin Shabani  akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi mitenje iliyopo kata mtipwili kuhusu ukatili wa kinjisia pamoja na haki za watotowakati wa utekelezaji wa kampeni ya mama samia msaada wa kisheria Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.                                        Mkurugenzi Msaidizi Wa haki za Binadamu ndugu Richard Kilanga akiongea na Wananchi wa kata ya Mtipwili Wilaya ya Nyasa wakati wa utekelezaji wa Kampeni ya Mama samia msaada wa kisheria.                                                  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George Mwakyembe – Nyasa Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Haki za binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheri

MAAMUZI YA MAHAKAMA HAYAANGALII UNYONGE WA MTU

Image
  Mhe. Jane Pascal Mudogo Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Nakapanya akitoa mada ya sheria kwenye utekelezaji wa Mama Samia Legal Aid Campaign Kata ya Nanjoka tarehe 24 Julai, 2023 Tunduru Bi. Blandina Adam Sekela Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tunduru akitoa mada ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Frank wilayani Tunduru, 24 Julai, 2023 Bi. Blandina Adam Sekela Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tunduru akiimba wimbo wa “usiniguse hapa” na wanafunzi wa shule ya Msingi Nanjoka wilayani Tunduru, 24 Julai, 2023. Mwanafunzi Salma Mbunya wa darasa la tano akiishukuru timu ya Mama Samia Legal Aid Campaign iliyofika shuleni hapo kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia na haki na wajibu wa mtoto, 24 Julai, 2023 Tunduru. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Tunduru Timu inayotekeleza Mama Samia Legal Aid Campaign Wilayani Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma imesema maamuzi ya Mahakama hayatolewi kwa kuangalia fulani ana uwezo na kumpa haki hata kama yeye ndiye mwenye makosa b
Image
  Wakili  Wa Serikari Bi. Jane Lyimo kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akitoa elimu ya sheria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Majengo, 23 Julai, 2023 Wilaya ya Tunduru. Bw. Kyema Paul Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Tunduru  akitoa mada ya ardhi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Majengo, 23 Julai, 2023 Wilaya ya Tunduru. Wakazi wa vijiji vya Majengo, Muungano na Kalanje wakifurahia kuwasili kwa timu ya Mama Samia Legal Aid Campaign kwenye ofisi za Kata ya Majengo, 23 Julai, 2023 Wilaya ya Tunduru. Na William Mabusi - WKS Tunduru Wakazi wa vijiji vya Majengo, Muungano na Kalanje wamewataka watumishi wa umma kutumia lugha nzuri kwa wananchi hasa pale wanapofika kwa ajili ya kupata huduma katika ofisi zao. Rai hiyo imetolewa na wananchi hao wakati wa utekelezaji wa Mama Samia Legal Aid Campaign wilayani Tunduru ambapo timu ya wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Wadau washirika walipofika katika vijiji hivyo kwa lengo la kutoa elimu na msaada wa kisheria l

PATIENI UFUMBUZI MASUALA AMBAYO NI KERO KWA WANANCHI: DKT. MPANGO

Image
 Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango  akihutumia  wananchi kwenye uzinduzi wa Kampeni  ya Mama  Samia  ya Msaada wa Kisheria  iliyofanyika Mkoani  Ruvuma Tarehe 22 Julai 2023.                                                         XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi & George Mwakyembe – WKS Songea Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka wataalamu wanaotekeleza Kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ijulikanayo kama Mama Samia Legal Aid Campaign kuyapatia ufumbuzi masuala wanayokutana nayo na kuonekana kuwa kero kwa wananchi wakati wa utekelezaji wa kampeni hiyo tangu ilipoanza Aprili mwaka huu ili watanzania wapate haki kwa wakati. Mhe. Mpango ameyasema hayo wakati akizindua utekelezaji wa kampeni hiyo mkoani Ruvuma tarehe 22 Julai, 2023 mjini Songea. “Fanyeni uchambuzi wa kina wa masuala mnayokutana nayo katika utekelezaji wa kampeni tangu ilipoanza kutekelezwa na kuyawekea mkakati wa kuyapatia ufumbuzi na kuweni tayari kuyabadili yale yatakayoonekana kuwa kero kwa wananc

NDUMBARO ATANGAZA NEEMA KWA WAANDISHI RUVUMA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na wahariri na waandishi 25 kutoka vyombo vya habari mjini Songea leo tarehe 19/07/2023 Mwezeshaji wa mafunzo hayo Dkt. Geofrey Chambua akitoa mafunzo kwa wanahabari walioshiriki warsha hiyo.  Mgeni Rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku - Ruvuma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameahidi kutoa zawadi nono kwa Waandishi watatu wa habari wa mkoa wa Ruvuma watakaofanya vizuri katika ushiriki, upashaji habari  na uhamasishaji wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria inayojulikana kama Mama Samia Legal Aid Campaign mkoani humo.  Waziri Ndumbaro ameyasema hayo tarehe 19/07/2023 mjini Songea Mkoani Ruvuma wakati akifungua mafunzo yaliyojikita kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari katika maeneo ya utafiti, uchambuzi na upashaji habari kwa masuala yanayohusu vitendo vya