Posts

Showing posts from May, 2023

MAHABUSU WALALAMIKIA VITENDO VYA RUSHWA MANYARA

Image
Timu ya wataalamu na uongozi wa gereza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kazi hiyo ya kutoa msaada wa kisheria kwa watu walio vizuizini.                                                        xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WKS MANYARA Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ameuagiza Uongozi wa Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Manyara pamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani humo kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mahabusu na Wafungwa wa gereza la Babati Mjini dhidi ya askari na watumishi wa vyombo hivyo vya haki ambapo katika nyakati tofauti wameonekana kutumia nafasi zao kudai rushwa kwa malengo ya kukwepesha haki. Tuhuma hizo zimetolewa tarehe 24/05/2023 wakati timu ya wataalam wanaoendesha Mama Samia Legal Aid Campaign ikiongozwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ilipofika gerezani hapo kwa lengo la kutoa elimu pamoja na msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa

MAKONDO AONGOZA TIMU YA UTOAJI MSAADA KISHERIA VIZUIZINI KONDOA NA CHEMBA

Image
  Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akikabidhi baadhi ya vifaa kwa ajili wafungwa na mahabusu wa Gereza la Kondoa.                                                   XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku – WKS Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo ameongoza timu ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali wanaoshiriki katika kampeni ya utoaji wa msaada na huduma za kisheria inayoitwa Mama Samia Legal Aid Campaign iliyotembelea katika maeneo ya vizuizi katika Wilaya za Kondoa na Chemba jana Tarehe 09/05/2023   Akiambatana na wataalam kutoka Ofisi ya Mashtaka, Tume ya Haki za Binadamu, Dawati la jinsia la Polisi, Wanasheria na watumishi wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Katibu Mkuu huyo alifika katika gereza la Kondoa na kufanikiwa kuongea na uongozi lakini pia na wafungwa na mahabusu waliokuwepo katika gereza hilo lengo likiwa ni kubaini changamoto za kisheria zikiwemo upatikanaji wa dhamana kwa wafungwa wanaostahili pamoja na namna kesi zao zinavyoendesh

KAMPENI YA MAMA SAMIA YATATUA MGOGORO BEREGE.

Image
  Mwenyekiti wa kijiji cha Berege ndugu Zebedayo Mchiwa akimshika mkono mwakilishi wa wananchi wa kijiji cha berege baada ya kupatanishwa na kumalizika kwa mgogoro uliotatuliwa na mafisa wanaotoa   msaada wa kisheria kwenye kampeni ya Mama Samia Legal Aid katika Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma.   Wananchi wa kijiji cha Berege Kata ya Berege Wilaya ya Mpwapwa wakiwa wanasikiliza elimu ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid Campain ambayo inatolewa na wataalaam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria. Kampeni hii imeanza tangu tarehe 28 aprili na kuhitimishwa tarehe 7 mei 2023.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe & Lusajo Mwakabuku – WKS  Mpwapwa.  Mama Samia Legal Aid Campaign inayoendelea mkoani Dodoma imekuwa msaada mkubwa katika kutatua matatizo mbalimbali katika jamii mbali ya kutoa elimu ya kisheria, pamoja na msaada wa kisheria. Hilo limethibitika katika kikjiji cha Berege kata ya Berege Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma baada ya kampeni hii kuwakutanisha wanakijij

DKT NDUMBARO AKEMEA UKATILI WA KINJISIA KONDOA

Image
         Mkazi wa Wilaya ya Kondoa akimweleza jambo Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro(hayupo pichani) Baada ya Waziri Ndumbaro kufanya ziara ya kukagua maenedeleo ya Mama Samia legal aid Campain  katika Wilaya ya Kondoa tarehe 6 mei 2023 jijini Dodoma.        Wananchi wa Wilaya ya Kondoa wakiwa wamejitokeza kwenye viwanja vya soko kuu kumsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro alipokuwa alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu Mama Samia Legal Aid Campain  tarehe 6 mei 2023 jijini Dodoma.  Mwananchi wa Wilaya ya Kondoa akimweleza Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro mgogoro wa ardhi baada ya Waziri Ndumbaro kufanya ziara ya kukagua maenedeleo ya Mama Samia legal aid Campain katika wilaya ya Kondoa tarehe 6 mei 2023 jijini Dodoma                xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na George Mwayembe – WKS Kondoa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro amekemea vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia unaojitokeza katika jamii zetu kwani licha ya

TAWLA yafanya Mkutano Mkuu wa 33

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akihutubia katika Mkutano Mkuu wa 33 wa TAWLA, tarehe 06 Mei, 2023   xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Mhe. Pauline Gekul Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ameshiriki ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tanzania Women Lawyers – TAWLA) uliofanyika tarehe 06 Mei, 2023 Jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi katika mkutano huo alikuwa Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania.  Katika hotuba yake Naibu Waziri, alisisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria itaendelea kushirikiana na TAWLA hususan katika kupokea mapendekezo na maoni ya marekebisho mbalimbali ya sheria.