Posts

Showing posts from December, 2023

UJENZI WA JENGO LA WIZARA WAFIKIA ASILIMIA 80

Image
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akiongea kwenye kikao na Mkandarasi wa jengo la Wizara kabla ya kutembelea na kukagua jengo hilo, tarehe 29 Desemba, 2023 Mji wa Serikali Mtumba. 0   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akitembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Wizara, tarehe 29 Desemba, 2023 Mji wa Serikali Mtumba. Mkandarasi Nasiri Nassoro akifafanua jambo wakati akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu alipotembelea na kukagua ujenzi huo, tarehe 29 Desemba, 2023 Mji wa Serikali Mtumba 01  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akishauri jambo alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Wizara, tarehe 29 Desemba, 2023 Mji wa Serikali Mtumba. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi -   WKS Dodoma Ujenzi wa jengo la Wizara ya Katiba na Sheria linalojengwa Mji wa Serikali Mtumba limefikia asilimia themanini (80).

DKT. CHANA ATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MASLAHI YA TAIFA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya RITA, 22 Desemba, 2023 Jijini Arusha. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya RITA, 22 Desemba, 2023 Jijini Arusha. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kwa kuzingata maslahi mapana ya Serikali na Taifa kwa ujumla. Dkt. Chana ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi ya RITA tarehe 22 Desemba, 2023 linalofanyika Jijini Arusha. Baraza hilo linafanyika ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya ajira na Mahusiano kazini. Amesema, “huduma ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu na Takwimu mnazotoa ni huduma zinazowagusa wananchi moja kwa moja. Hivyo, mkiwa wafanyakazi mlioaminiwa na Serikali ya Tanzania endele

DKT. CHANA APOKEA CHETI CHA HESHIMA KUTOKA TAASISI YA KUPINGA RUSHWA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana atunukiwa tuzo kutoka kwenye Taasisi ya Anti Corruptions Voices Foundations kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu tarehe 10 Desemba, 2023 Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amepokea cheti cha heshima kutoka Taasisi ya Kupinga Rushwa (Anti Corruptions Voices Foundations) alichotunukiwa kutokana na kuwa Mgeni Rasmi katika mbio za “Sepesha Rushwa Marathon.” Balozi Chana amekabidhiwa cheti hicho tarehe 10 Desemba, 2023 wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na   Haki za Binadamu.

Wananchi watakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu

Image
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika banda la Wizara ya Katiba na Sheria kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika leo tarehe 10 Desemba 2023 Jijini Dodoma.  Mgeni rasmi Mhe. Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wengine meza kuu kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu  yalifanyika leo tarehe 10 Desemba 2023 jijini Dodoma. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba kwenye Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika leo tarehe 10 Desemba 2023 Jijini Dodoma. Watumishi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali wakimsikiliza Mhe. Waziri Mkuu Kass im Majaliwa alipokuwa akihutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika leo tarehe 10 Desemba 2023 Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Balozi Pindi Chana akitoa neon la utambulisho kwenye Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika leo tarehe 10 Desemba 2023 Jiji

TANZANIA IMESAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO ZAIDI YA MILIONI NANE

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya miaka mitano, Desemba 08, 2023 katika viwanja vya Mbagala Zakhiem Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizira ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya miaka mitano, Desemba 08, 2023 katika viwanja vya Mbagala Zakhiem Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizindua Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya miaka mitano, Desemba 08, 2023 katika viwanja vya Mbagala Zakhiem Jijini Dar es Salaam. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku - DSM Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa Watoto zaidi ya milioni 8.8 wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara kupitia Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya miaka mitano. Mhe. Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana a

“UNYANYASAJI WA KIJINSIA HAUNA NAFASI KATIKA NCHI YETU” DKT. CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati akifungua Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, tarehe 06 Desemba, 2023 Jijini Dodoma. Washiriki siku ya kufungua Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, wakimkaribisha ukumbini Mgeni Rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana tarehe 06 Desemba, 2023 Jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki hafla ya kufungua Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, tarehe 06 Desemba, 2023 Jijini Dodoma.                                    XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Tanzania inaweza kusonga mbele na kushinda vita dhidi ya Ukatili wa Kijinsia ikiwa wote tutazungumza na kupaza sauti kupinga Unyanyasaji wa kijinsia huku akiitaka jamii kushiriki kikamilifu katika kutoa ushahidi wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia mara inapo

NCHI IKITAWALIWA NA RUSHWA HAIWEZI KUFIKIA MALENGO: BI. MAKONDO

Image
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akihutubia kwenye Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa juhudi dhidi ya rushwa, tarehe 04 Desemba, 2023 Jijini Dodoma. Washiriki kwenye Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa juhudi dhidi ya rushwa, wakisikiliza hotuba, tarehe 04 Desemba, 2023 Jijini Dodoma. Meza Kuu kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Serikali kwenye Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa juhudi dhidi ya rushwa, wakisikiliza hotuba, tarehe 04 Desemba, 2023 Jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na William Mabusi – WKS Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amezitaka Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi kuweka mazingira ya kuzuia rushwa, kuepuka na kutokomeza vitendo vya rushwa nchini ili kuliwezesha taifa kufikia malengo mbalimbali iliyojiwekea katika kuleta maendeleo nchini. Bi. Makondo ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa juhudi dhidi ya rushwa tarehe 04 Desemba, 2023 Jijini Dodoma lililo hudhuriwa n

KUPIGA VITA RUSHWA NI JUKUMU LETU SOTE – MHE. PINDI CHANA.

Image
    Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pindi Chana akiongea na Wananchi kwenye  Uzinduzi wa Maadhimisho ya   ya siku ya Maadili  na Haki za Binadamu  Kitaifa yalifanyika uwanja wa Jamhuri leo tarehe 03 Desemba 2023  Jijini Dodoma Waziri wa katiba na sheria Mhe. Pindi Chana akiwa na viongozi  meza kuu  kwenye Uzinduzi wa Maadhimisho ya   ya siku ya Maadili  na Haki za Binadamu  Kitaifa yalifanyika uwanja wa Jamhuri leo tarehe 03 Desemba 2023  Jijini Dodoma  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa mbio za Sepesha Rushwa Marathoni   kilomita 21  kwa upande wa wanawake leo tarehe 03 Desemba  2023 Jijini Dodoma.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe – WKS Dodoma.   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa uwepo wa vitendo vya rushwa kunaifanya Serikali kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, kushindwa kuwahudumia wananchi, miradi ya maendeleo  kushindwa kufanyika au kufanyika kwa kiwango

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA UPATIKANAJI HAKI NCHINI INDIA

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pindi Chana  akiwa na wajumbe kutoka Tanzania   kwenye  Mkutano wa Upatikanaji Haki uliofanyika tarehe 27- 28  New Delhi,  India . XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na, George Mwakyembe - WKS Tanzania ni moja kati ya nchi washiriki katika mkutano wa kwanza wa kikanda kuhusu upatikanaji wa msaada wa kisheria, pamoja na Uimarishaji wa upatikanaji Haki katika nchi za ukanda wa kusini. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameongoza washiriki kutoka Tanzania katika mkutano huo uliofanyika New Delhi nchini India kuanzia tarehe 27– 28 Novemba 2023 ukiwa unalenga kujadili masuala ya upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria katika kuimarisha upatikanaji haki nchini. Katika Mkutano huo washiriki walipata nafasi ya kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa masuala ya huduma za msaada wa kisheria na jitihada mbalimbali zinazotumika katika kuhakikisha upatikanaji haki katika nchi zao pamoja na kuimarisha uhusiano na   baina   nchi washiriki na