Posts

Showing posts from December, 2022

DKT. NDUMBARO ASHIRIKI HAFLA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU WA KENYA

Image
XXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax katika Hafla ya maadhimisho ya miaka ya 58 ya Uhuru wa Taifa la Kenya yaliyofanyika tarehe 12/12/2022, Jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahaman Kinana, Amidi wa Mabalozi wa mataifa mbalimbali Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui. Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kenya, ni fursa pekee ya kuangalia mahusiano baina ya nchi hizo mbili ambapo siku zote yamezidi kuimarika kama yalivyoasisiwa na Waasisi wa Mataifa haya mawili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Jomo Kenyatta. Aidha, Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa pamoja na kwamba mahusiano katika Nyanja za Biashara yamezidi kuimarika zinahitajika jitihada zaidi na kutoa rai kwa wafanyabiashara kue

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA MAAFISA KUTOKA UBALOZI WA UINGEREZA

Image
  XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na maafisa kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini; Dkt. Zabdiel Kimambo -Mshauri wa Utawala, Bw. Laurence Wilkes, Mshauri wa Masuala ya Utawala na Siasa, na Bi. Allanna Inserra, Mshauri wa Masuala ya Siasa tarehe 14 Desemba, 2022 katika Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho wamejadili masuala mbalimbali yahusuyo ushirikiano baina ya Serikali na Asasi za Kiraia na utekelezaji wa miradi ambayo inafadhiliwa na Uingereza kupitia Asasi mbalimbali hapa nchini. Dkt. Ndumbaro ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuwa na ushirikiano na uhusiano mzuri na Asasi za Kiraia hususan katika upatikanaji wa maoni katika sheria mbalimbali zinazohitaji kufanyiwa marekebisho.  Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Casmir Kyuki na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Griffin Mwakapeje. Kwa u

DKT. DAMAS DUMBARO AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU

Image
  XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.  Damas Ndumbaro amezindua maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Bindamu kitaifa.  Maadhimisho hayo yamezinduliwa  tarehe 6 Desemba, 2022 katika viwanja vya Nyerere Square vilivyopo katikati ya mji,  jijini Dodoma.  Akiongea kwenye  Uzinduzi   huo Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema "Maadhimisho haya yameanza mwaka 2016  kwa lengo la kuwa na siku ya kimataifa ya kupambana na Rushwa pamoja na siku ya kimataifa ya Haki za Binadamu  ili kuwaelimisha wananchi namna ya kupiga vita rushwa  na  pia  juu ya masuala ya Haki za Binadamu." Pia Dkt. Ndumbaro amesema "Jukumu kubwa la Serikali yetu ni kuwaletea Wananchi  maendeleo, hivyo Usimamizi wa Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Uwazi na mapambano dhidi ya rushwa  ni masuala endelevu kwa kuwa ni msingi wa utoaji huduma bora kwa Umma." Kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema _"Maadili, Haki za Binadamu, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa ni jukumu la pamoja ka

HATUA KALI ZAIDI KUCHUKULIWA KWA WAHALIFU WA MAKOSA YA UNYANYASAJI KIJINSIA: DKT. NDUMBARO

Image
XXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali imejipanga kuchukua hatua kali zaidi kwa wahalifu wa makosa ya unyanyasaji kijinsia. Waziri Ndumbaro ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) Novemba 5, 2022 Jijini Dar es Salaam. Dkt. Ndumaro amesema “rai ya Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kupaza sauti siku zote 365 za mwaka kutambua viashiria vya unyanyasaji wa kijinsia na kuvitolea taarifa kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake.” Katika hatua nyingine Mhe. Ndumbaro amesema “Wizara ya Katiba na Sheria iko mbioni kuanzisha usajili wa mtandaoni (online registry) kwa mtu ambaye amethibitishwa na Mahakama kuwa na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia.” Watu watakaokuwa katika orodha hiyo hawatakuwa na uwezo wa kukopa benki wala kupata ajira, miongoni mwa huduma zingine. Kwenye maadh