Posts

Showing posts from March, 2023

“ARUSHA NI MJI WA KIMATAIFA WA SHERIA” - NDUMBARO

Image
Waliokaa ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro akiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari Mhe. Jaji Graciela Gatti Santana pamoja Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Joseph Mhagama(Mb), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul na Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo na viongozi wengine wa Wizara na Mahakama ya Kimbari katika picha ya pamoja.                                      XXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe, Lusajo Mwakabuku na Nkasori Sarakikya - WKS Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (UN-International Residual Mechanism for Criminal Tribunals), iliyopo Arusha Jaji Graciela Gatti Santana leo tarehe 28 machi 2023 jijini Dodoma. Akiongea kwenye kikao hicho Mhe. Ndumbaro Alieleza umuhimu wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari - Rwanda (UN-Int

Mhe. Pauline Gekul amewataka waajiriwa wapya kuwa na uweledi

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amewataka waajiriwa wapya kuwa na uweledi, kuepuka vitendo vya ukiukaji wa maadili ya kazi pamoja na kuepuka rushwa, uonevu na matumizi mabaya ya ajira zao. Mhe. Gekul aliyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, yaliyofanyika Mkoani Morogoro, Hoteli ya Kingsway kuanzia tarehe 17-23 Machi, 2023.

Wizara 23 zaungana kutokomeza TB

Image
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Marry Makondo pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, na Uratibu  Dkt Jim Yonazi  wakiwa  kwenye picha ya pamoja  na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali  baada ya kikao  tarehe 21 Machi 2023 Jijini Dodoma .                                                                                                             xxxxxxxxxxxxxxxx  Na, Lusajo Mwakabuku. Katika kuhakikisha dhamira ya kupambana na hatimaye kuitokomeza TB na vichochezi vyake inakamilika, ushirikiano wa Sekta mbalimbali za Serikali zaidi ya zile zinazohusika na afya pamoja na vipaumbele thabiti vya kisiasa katika ngazi za juu za uongozi vina nafasi kubwa katika kuumaliza ugonjwa huu nchini. Ni kwa mtazamo huo wa Serikali uliopelekea Wizara 23 kuingia makubaliano ya kuunda Mfumo wa Uwajibikaji wa Sekta mbalimbali ( Multisectoral Accountability Framework - MAF ) uliotiwa Saini na wawakilishi wa Wizara hizo jana 21/03/2023 Jijini Dodoma.

NAIBU WAZIRI AFANYA ZIARA RITA

Image
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Pauline Philipo Gekul (Katikati)  katika picha ya pamoja  na baadhi ya  Watumishi  na Menenjimenti ya RITA  tarehe  17 Machi, 2023 Jijini Dar es salaam.                                                 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku & Josephat Kimaro Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Pauline Philipo Gekul (Mb) leo Machi 17, 2023 amefanya ziara na kuzungumza na Menejimenti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA). Kupitia ziara hiyo, Mhe. Gekul amepokea taarifa ya utekelezaji pamoja na kujengewa ufahamu kuhusu kazi na majukumu ya Wakala ya kuwahudumia Wananchi kutoka kwa Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi. Angela Anatory. Mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Mhe. Naibu Waziri ameipongeza RITA kwa mageuzi makubwa wanayofanya kwa kuwezesha wananchi kuweza kutuma maombi ya huduma kidijitali popote walipo bila kufika katika ofisi za Wakala. Pia akaitaka

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIMWAGIA SIFA MAHAKAMA

Image
 Mtendaji  wa Mahakama Kuu ya Tanzania  Bw. Leonard  Magacha( Kulia )  akimwonesha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Katiba na Sheria (Mb) na Wajumbe wa Kamati hiyo alioambatana nao kwenye ukaguzi  wa ukarabati  wa jengo la Mahakama liliokuwa  likitumika kama ofisi ya  Serikali za Mitaa. Tarehe 14  Machi, 2023 Mjini Tabora.                                            xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx  Na Lusajo Mwakabuku – WKS Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imekagua Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora na kuridhishwa kwa kazi inayofanywa na Mahakama katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya majengo yake.  Mara baada ya ziara hiyo ya siku moja ya ukaguzi wa utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora iliyofanyika tarehe 14 Machi, 2023, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria,

DKT. NDUMBARO MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA UDOM

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria  Mh. Damas Ndumbaro  akiwa katika mazungumzo  na Dkt Ines Kajiru  pamoja na timu yake  tarehe 13 machi katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria, Mtumba Jijini Dodoma.   Dkt Damas Ndumbaro  Waziri wa Katiba na Sheria kwenye picha ya pamoja na Dkt Ines Kajiru  pamoja na timu yake tarehe 13 machi  2023 ofisi  za Wizara, mtumba Jijini Dodoma.                                                                 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx  George Mwakyembe & Lusajo Mwakabuku - WKS Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekubali mwaliko wa kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Sheria yanayotarajia kufanyika tarehe 24 Machi 2023 katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Kauli hiyo imetolewa na Amidi wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt. Ines Kajiru alipokutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Waziri Ndumbaro leo tarehe 13 Machi 2023 katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria za Mtumba Jijini Dodoma. Aidha, Dkt Kajiru alimweleza Mhe. Wa

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAELEKEZA LUGHA ZA KIINGEREZA NA KISWAHILI KUTUMIKA WAKATI WA UTUNGAJI WA SHERIA.

Image
Sehemu ya wanakamati  wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria  na Viongozi  wa Taasisi za Wizara hiyo wakifuatilia  aarifa  ya Mhe. Waziri Ndumbaro. Wazir wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro  akiwasilisha taarifa  inayohusu Muundo  na Majukumu ya Wizara  pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria  kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala , Katiba naSheria  Tarehe 12 Machi 2023.   Katibu Mkuu  wa Wizara ya Katiba na Sheria  Bi. Mary Makondo ( Mbele kushoto)  akiandika  maelekezo ya yaliyokuwa yakitolewa na wajumbe wa Kmati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria  Baadhi ya wajumbe  wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Utawala, Katiba na Sheria   wakifuatilia mazungumzo  wakati wa kikao cha Wizara ya Katiba na Sheria  na Kamati ya Kudumu ya ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria .                                                    xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na George Mwakyembe & Lusajo Mwakabuku – WKS. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawa

Wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria washiriki maadhimisho ya siku ya Wanawake

Image
  Watumishi wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wakishangilia kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.                              XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Wafanyakazi wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wameadhimisha siku ya Wanawake Duniani Kwa kuungana na wanawake wengine kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi katika maadhimisho hayo kimkoa yaliyofanyika katika Wilaya ya Kondoa. Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 08, 2023 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rosemary Senyamule. Watumishi hao wameshiriki kwenye maandamano yaliyopokelewa na Mgeni Rasmi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali. Dkt. Senyamule wakati akiongea na watumishi wanawake kutoka ofisi mbalimbali amewaasa kujiamini na kuwa imara ili waweze kutimiza malengo yao bila kusubiri kusukumwa kwani uwezo wanao wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya jamii yao. Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani

SERIKALI YAJIVUNIA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO

Image
  Picha ya pamoja  ya meza kuu  na  wajumbe wa Menejimenti ya Chuo cha Uongozi  wa Mahakama  Lushoto  pamoja na Watumishi  wa chuo hicho.                                xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Lusajo Mwakabuku & Felix Chakila - WKS Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto - IJA ni chuo cha mfano wa kuigwa katika utoaji wa mafunzo elekezi ya awali na mafunzo endelevu ya kimahakama kwa kuzingatia Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya Mwaka 2019 ambayo inakitambua Chuo hicho kama kitovu au kisima cha utoaji mafunzo kwa watumishi wa Mahakama. Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo Tarehe 6 Machi, 2023 alipotembelea Chuo hicho na kuzungumza na Uongozi wa Chuo, Menejimenti ya watumishi na Wafanyakazi wa IJA na kuongeza kwamba Wizara ya Katiba na Sheria inajivunia kwa uwepo wa chuo hicho ambacho kimebeba taswira ya nchi hususan kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kimeendelea kuwa mfano wa kuigwa kama Chuo kinacho

DKT NDUMBARO AZINDUA KANUNI ZA WATOA TAARIFA

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria  Dkt. Damas Ndumbaro  akizindua  Kanuni za Watoa Taarifa  na Ulinzi  wa Mashahidi,  tarehe  28 Februari 2023, Kulia Naibu Waziri Pauline Gekul  na  Kushoto Naibu Katibu Mkuu Khatibu Kazungu.                                 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Mwandishi wetu, Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amezindua Kanuni za Watoa Taarifa na Ulinzi wa Mashahidi za mwaka 2023 na kueleza kuwa Kanuni hizo zitasaidia kufichua uhalifu na kuimarisha utoaji haki jinai. Dkt Ndumbaro ameyasema hayo wakati wa kuzindua Kanuni hizo hatua ambayo inaashiria kuanza utekelezaji wa Sheria ya Watoa Taaarifa na Ulinzi wa Mashahidi ya mwaka 2016. Katika uzinduzi huo ambao umefanyika tarehe 28 Februari, 2023 Dkt Ndumbaro amesema kanuni hizo zinaenda kusaidia uimarishaji utoaji wa haki jinai kwa sababu zinahusu utoaji wa taarifa za ukiukwaji wa sheria mbalimbali, makosa ya jinai, wizi wa mali za umma na ufisadi. “Watoa taarifa hizi ni muhimu sana kwenye