Posts

Showing posts from February, 2024

BUNGE LARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO INAYOTOA KWA SERIKALI

Image
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akisoma Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika kipindi cha kuazia Februari, 2023 hadi Januari, 2024. Tarehe 13 Februari, 2024 Bungeni Dodoma. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akijibu mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, tarehe 13 Februari, 2024 Bungeni Dodoma. Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Michael Masanja akimkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda kuongea na Wataalamu wa Wizara kujadili majibu ya mapendekezo ya Bunge, tarehe 13 Februari, 2024 Bungeni Dodoma. Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Katiba na Sheria walioshiriki katika kikao cha kuandaa majibu ya mapendekezo ya Bunge, tarehe 13 Februari, 2024 Bungeni Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

MAWAZIRI WA SHERIA KUTOKA JUMUIYA YA MADOLA KUTIRIRIKA TANZANIA – DKT. CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na Wandishi wa Habari Ofisi za Bunge, 07 Februari, 2024 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kuongea na Wandishi wa Habari Ofisi za Bunge, 07 Februari, 2024 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na Wandishi wa Habari Ofisi za Bunge, 07 Februari, 2024 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Pindi Chana amesema maandalizi ya Tanzania kupokea Mawaziri wa Sheria wa nchi 56 Wanachama wa Jumuiya ya Madola wakiambatana na Maofisa wao Waandamizi yamefikia mwishoni na hivyo Mawaziri hao kuanza kutiririka Nchini kuanzia Machi 04, 2024. Dkt. Chana ameyasema hayo leo tarehe 07 Februari, 2024 alipofanya mkutano na Wandishi wa Habari Bungeni Jijini Dodoma kueleza maandalizi ya Mkutano huo. “Maandalizi ya Mkutano huo yanafanywa na Wizara ya Katiba

BAJETI ZIZINGATIE UTEKELEZAJI WA 4R ZA MHE. RAIS – DKT. CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea alipokutana na Wakuu na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara, tarehe 06 Februari, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma. Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Bw. George Mandepo akitoa wasilisho fupi la maoteo ya bajeti ya Taasisi yake kwa mwaka wa fedha 2024/25, tarehe 06 Februari, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma. Kabidhi Wasii Mkuu ofisi ya RITA Bw. Frank Kanyusi akitoa wasilisho fupi la maoteo ya bajeti ya Taasisi yake kwa mwaka wa fedha 2024/25, tarehe 06 Februari, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameziagiza Taasisi za Wizara hiyo kuhakikisha zinazingatia pamoja na mambo mengine ya maendeleo lakini pia utekelezaji wa R4 za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Dkt. Chana ametoa agizo hilo wakati alipokutana na Wakuu wa Taasisi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara, Wakurugenzi kutoka Wizarani na kupitishwa kwenye

IGUNGA KUPATA JENGO JIPYA LA MAHAKAMA YA WILAYA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akijibu swali Bungeni, tarehe 06 Februari, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali imepanga kujenga jengo la Mahakama ya Wilaya ya Igunga katika mwaka wa fedha 2024/25. Dkt. Chana amesema hayo tarehe 06 Februari, 2024 Bungeni alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Igunga   Mhe. Nicholaus George Ngassa aliyetaka kujua lini Serikali itajenga jengo la Mahakama ya Wilaya ya Igunga. “Igunga ni moja ya Wilaya ambazo hazina jengo la Mahakama ya Wilaya kwa muda mrefu. Kwa sasa Mahakama ya Wilaya inafanya kazi ndani ya jengo moja na Mahakama ya Mwanzo Igunga mjini, jengo ambalo lilijengwa kwa ajili ya Mahakama ya Mwanzo. Kwa kuzingatia Mpango wa ujenzi wa Mahakama, jengo la Mahakama ya Wilaya ya Igunga linatarajiwa kujengwa katika Bajeti ya Mwaka 2024-25.” Amesema.

TUNAANDAA MKUTANO WA VIWANGO VYA JUU – DKT. CHANA

Image
  Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amepitishwa kwenye taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Sheria kutoka nchi za Jumuiya ya Madola, tarehe 05 Februari, 2024 Dodoma na kuahidi “Tutafanya Maandalizi mazuri na kwa Viwango vya Kimataifa kwa heshima ya Nchi yetu.” xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amepitishwa kwenye taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Sheria kutoka nchi za Jumuiya ya Madola, tarehe 05 Februari, 2024 Dodoma na kuahidi kuandaa mkutano utakaokuwa wa viwango vya juu kwani tayari uwezo wa kuandaa mikutano ya kimataifa Wizara unao ambapo mwishoni mwa mwaka 2023 Wizara iliratibu kikao cha 77 cha Kamisheni ya Haki za Binafamu kilichofanyika mkoani Arusha kwa siku 21. “Tutafanya Maandalizi mazuri na kwa Viwango vya Kimataifa kwa heshima ya Nchi yetu.” Alisema Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Katiba na Sheria akilezea mkutano huo utakaofanyika kuanzia tarehe 04 – 08 Machi, 2024 Zanzibar.

WIZARA KUENDELEA KUBORESHA SHERIA – DKT. CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akijibu maswali, tarehe 02 Februari, 2024 Bungeni Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria itaendelea kuzifanyia utafiti na kuboersha sheria zote zinazotakiwa kufanyiwa mabadiliko. Dkt. Chana amesema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Emmanuel Adamson Mwakasaka, aliyetaka kujua lini Serikali italeta Bungeni Sheria mahsusi kwa ajili ya kuwalinda wananchi dhidi ya Ukatili wa Kijinsia. Amesema “tunazo Sheria zinazowalinda wananchi dhidi ya ukatili wa kijinsia ambazo ni Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, Sheria ya Ndoa Sura ya 29, Sheria ya Mtoto Sura ya 13, Sheria ya Makosa ya Mtandao Sura ya 443 na Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Sura ya 432. Kwa pamoja Sheria hizo zina vifungu vinavyozuia makosa ya ukatili wa kijinsia, zote kwa pamoja zina vifungu vinav

TEKELEZENI KWA UKAMILIFU MFUMO WA UTOAJI MSAADA WA KISHERIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Siku ya Sheria, tarehe 01 Februari, 2024 Jijini Dodoma.   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (katika), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Mustapher Siyani kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria, 01 Februari, 2024, Jijini Dodoma. Bi. Mary Makondo Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria, 01 Februari, 2024, Jijini Dodoma. Bi. Mary Makondo Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Viongozi wengine wakifurahia jambo kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria, 01 Februari, 2024 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wadau wengine k